''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 15, 2014

MKUMBUKE MKEWE LUTU

Mhubiri: Mrs. Lucy Masembo 
MAANDIKO: Luka 17:32 

Wewe binafsi mkumbuke mkewe lutu, kwanini Yesu alisema mkumbuke mkewe lutu, tunapokumbuka mambo mazuri yanafanya tuendelee mbele na mambo mabaya yanafanya tujirekebishe na tuendelee mbele. Lutu alikuwa ni ndugu yake ibrahimu, ibrahim alitoka kwao na lutu, na huko mbeleni ibrahim alipo barikiwa baraka zile zilimpata na lutu na mifugo yao ikawa mingi na wachunga wa mifugo yao wakataka kugombana lakini ibrahim akamwambia wasigombane bali lutu achague eneo la kwenda, lutu mwenyewe akainua macho akaona bonde zuri la malisho akachagua huko, lutu aliangalia kwa macho ya kawaida akaona ni pazuri wala hakuomba ili Mungu amuongoze kwahiyo alichagua kwa kutumia akili zake mwenyewe na kuona ni pazuri kumbe huko mbeleni ikawa ni nchi mbaya yanye maovu mengi, na walipofika nchi ilie hali ya kiroho ya lutu inavyooonekana ilipungua sana, baada ya muda malaika wakamjia ibrahim wakasema tunaenda kwa lutu nduguyo ibrahim akaomba sana ili isiangamizwe ile nchi. 

Hapa tunaweza kujifunza kuwa wanaume katika familia Mungu amewafanya kuwa viongozi kwahiyo wanatakiwa kuongoza mahali pazuri, lutu alichagua sehemu ambapo badae familia yake nzima ilipata shida. Malaika walipofika kwa lutu watu wa nchi ilie walisema watoe hao watu waliokuja wakafanya vurugu malaika wakawapiga upofu malaika wakathibitisha kuwa mambo hayaendi vizuri. 

Mkewe lutu alikuwa na fursa zote za kuweza kuponya 1. aliwaona malaika na vitu vyote walivyovifanya kupiga upofu, sasa pamoja na kuona mambo malaika waliyoyafanya katika nyumba yake lakini hakuzingatia hakuamua kubadilika, unajua angeweza kujibadilisha na kuamini walichosema wale malaika unaweza kusoma Mwanzo 19:12-17 aliona hata lutu alipotoka kuongea na wakweze lakini aliona kawaida tu kama siku hizi wengi wanapochukulia kawaida tu roho mtakatifu anapoongea nasi, wakati huu sio salama pia 2.mkewe lutu alihimizwa mwamzo 19:16-17, 3.aliambiwa jiponye nafsi yako usitazame nyuma na usisimame kwenye hilo bonde luka 19:17 jiponye nafsi yako na jambo kubwa waliambiwa usitazame nyuma, labda mkewe lutu alikuwa anajiuliza kwanini nasema nisitazame nyuma labda moyo wake ulikuwa bado lutu, inawezekana unajiuliza imekuwaje namimi nimeokoka kwanini nisirudi nyuma kunywa pombe au kufanya starehe flani, usikumbuke mambo mabaya, 

2. pia huyu mkewe lutu hakuwa tayari kuhamishwa rumi 12, 1petro 4:2-4, kuna mambo ambayo watu wa kule duniani hawategemei mambo flani uyafanye mtu uliyeokoka, waliambiwa msitazame nyuma lakini tunaona mkewe lutu hakuwa mtii kwa maagizo aliyopewa alitazama nyuma akawa jiwe la chumvi, 

3. hakuwa mkweli kwa nafsi yake mwenyewe, unajua mtu anaweza kusema nakupenda lakini hujui ndani yake ana mambo gani juu yako, ukiamua kuokoka amua kweli usijidanganye mwenyewe, lutu aliamua kubadilika ndio alichagua vibaya, lakini kwa muda ule hakuchezea nafasi ilie akaenda hakusimama wala halkuangalia nyuma, jidhibitisheni mwenyewe kuwa uko sama katika wokovu, 1korith 11, mkewe lutu alijifanya anatoka, jiponye nafsi yako mwenyewe, simama kwa miguu yako tembena kwa miguu yako, kubali kuonywa, kwa wamama usipotii maagizo ya mume wako usipotii utakufa anapokwambia hivi alafu wewe unasema nitafanya hivi hiyo ni dhambi. wale malaika hawakusema jiponyeni lakini walisema jiponye yaani wewe binafsi ujiponye hali ya sasa ni mbaya, jiulize unafanye kila kitu, je unaoaje? au Unaolewaje?, .. kwanini tumkumbuke lutu, ni kwasababu alichezea nafasi aliopewa, nafasi ya wokovu uliyonayo ni ya thamani mno usiichezee usichezee wokovu, esau nae aliuza uzaliwa wa kwanza, lakini badae esau alijuta, mungu amekuchagua wewe upate wokovu kwahiyo jiangalie nafsi yako, tusiipende dunia namambo yake, sahv tunaonywa mno lakini sio wote wanaoacha, jingne ukirudi nyuma utapata hasara, jiponye nafsi yako usije ukarudi nyuma, 1koritho 10:1-7 hasa mstari wa 5-7, jumkini unaona haya si maneneo ya kilia siku lakini ni kweli yapo kwahyo tuamua kubadilika. kumbuka wapi ulipoanguka, jipnye nafsi yako bcz bado unayo nafasi ya kupona.

Mrs. Masembo akihubiri

No comments:

Post a Comment