''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 22, 2014

UTOAJI WA MUNGU WETU ALIYE HAI

MHUBIRI: Mchungaji Kiongozi Mhini.
MAANDIKO: 1wafalme 17:1-16, Mathayo 6:25-34 

Baada ya Mungu kuumba ulimwengu hakuacha ulimwengu ukae peke yake bali aliumba na vitu vingine ili vitusaidie, Mungu ndiye anayekupa mahitaji yako, Yesu ndiye anayekupa mahitaji yako, sasa ujumbe huu ni wa kutia moyo wewe ambaye unapitia kipindi kigumu Mungu yupo na anaweza kukusaidia. 

Mungu akamuamuru Elia amtembelee mjane huyu, Mungu alimpa mahitaji yake yote kwasababu Elia alimtumukia Mungu, tambua kuwa kumtumikia Mungu kuna faida nyingi sana, Mungu alishughulika na mahitaji ya Elia kwasababu alikuwa ni mtumishi wake, hebu jiulize wewe mwenyewe Je wewe unamtumikia Mungu? amua kumtumikia Mungu kwanzia leo na Mungu atahusika na mahitaji yako.

Yawezekana uko njia panda na huelewi ufanyeje matatizo ni mengi lakini usihofu Mungu  atatuma kunguru kwahiyo usiwe na wasiwasi Mungu yuko pamoja nawe lakini hakikisha  uwe tu na imani. 

Haijalishi uko kwenye hali gani lakini Mungu ana sifa zifuatazo 
1. Mungu anatunza 
2. Mungu anatupa mahitaji yetu 
3. Mungu anaongoza 

Ni kweli tunapitia katika changamoto tofauti tofauti, ni kweli katika dunia hii kuna matatizo na kuna siku utapata matatizo lakini swali ni Je tegemeo lako ni nini? je unategemea watu wa dunia hii? nakushauri tegemeo lako liwe  kwa Mungu, endela kuomba kwa bidii, Elia aliendelea kuomba kila siku kwa bidii. Ni kweli watu tuna mahitaji tofauti tunatofautiana kwneye mahitaji yetu, mwengine anahitaji hela, mwengina anahitaji uponyaji kwahiyo uombaji wetu utakuwa tofauti lakini mmpaji wetu ni mmoja naye ni Yesu Kristo. Katika Neno hili tunaona Elia alipewa chakula na kunguru na ukisoma Warumi 8:28 tunaona Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Kwahiyo wewe kama mwanadamu na mahitaji yote uliyonayo unaye baba ambaye kwake wote tupo sawa hakuna hata mmoja ambaye sio muhimu kwa Mungu, Mungu wetu anatujali wote kama watoto wake, ndomana tunasema Mungu ndio mmpaji wetu atatupa kila unachohitaji kumbuka kwamba hauko peke yako na kwasababu Yesu anakupenda upendo wa Mungu haiutegemei jinsi unavyoonekana. Matatizo yapo lakini mtegemee Yesu, inawezekana unamtumikia Bwana lakini unaweza kujiuliza kwanini mabaya haya yanakupata? kwanini mabaya haya yakukute? lakini kumbuka shida zipo cha muhimu ni kumbuka wapi pa kuombea msaada, unapoenda kwa Bwana na kumuomba msaada ataonekana kwako kwa haraka sana, tunaye Mungu anayehisi matatizo yako, anayehisi pamoja nasi anaumia watoto wake wanapoumia, pia kumbuka kuna ushindi, na kuna kunguru atakaye kulisha kwa muda muafaka, mchagua Yesu kuwa kimbilio lako pia kumbuka ukimtumikia Bwana Yesu ushindi upo. Nakutia moyo Mungu yupo kazini anafanya kazi 24/7 kuhakikisha usalama wako. Kumbuka anayekupa mahitaji yako ni Yesu, Yeye anayekupenda sana, usilalamike Yesu yuko kwaajili yako. Inawezekana una matatizo ya kindoa lakini mkimbilie Mungu. Mungu anahusika kabisa na mtu mtakatifu. Kaa kwenye Neno umuone Mungu.
Mch. Mhini na mtafsiri wake Mr.Benard Okech


 -------------------------------------------------------------------------------------------------

WATU WA (4)NNE WAMPA YESU MAISHA YAO 


KIPINDI CHA KUSIFU NA KUABUDU


No comments:

Post a Comment