Mhubiri: Mchungaji Kiongozi Meshark Mhini
Maandiko: 1Petro 2:21,Luka 2:52,Warumi 8:29,Matendo 3:14,Yohana 14:31,Marko
6:34-44
Kuishi ni kuishi tu, lakini
unaishije, je unaishi kwa viwango vya ki-Mungu? je unatambua nani ni mmumbaji
wako? Je unatambua nani ni mwokozi wako?. Hapa Tanzania tuna shirika la kuangalia viwango (TBS)
wanacheki bidhaa mbalimbali kama bidhaa hazijafikia viwango zinaweza zuiliwa na
kwa Mungu kuna viwango vya ki-Mungu, swali kwako, Je wewe unaishi maisha ya viwango vya
ki-Mungu? hata kwa Mungu kuna viwango vya kuishi maisha ya Ki-Mungu, jiangalie kama wewe una viwango vya chini badilisha viwango vyako , jiangalie mwenyewe na ujione upo kwenye viwango gani na uviongeze. Je unaishi maisha yaliyo kwenye viwango vya ki-Mungu au uko chini ya viwango? Na bahati nzuri tunajazwa Roho Mtakatifu ambaye ukienda vibaya anakwambia hapa umenda vibaya unashuka viwango kwahiyo unafanya mabadiliko.
Sisi mfano wetu ni Yesu, fuata viwangu vya Mungu, Yesu ndio kielelezo
chetu Luka 2:52. Fuata tabia Yesu alizozifundisha? 1petro 2:21, Wewe
kama mtu uliyaokoka lazima ufuate tabia za Yesu. Sasa jiulize maisha yako yanafanana na maisha ya
viwango vya ki-Mungu? Warumi 8:29, Matendo 3:14, Yesu alikaa kimya ni kwasabau alifuata tabia za baba yake na wewe
fuata na ishi kama Mwokozi wako Yesu Kristo wa nazareti aliye hai, acha kutenda dhambi, ishi maisha ya kumpendeza Mungu, Yohana 14:31, Yohana 6:38-40. Yesu alijikana kwa ajili yetu na hataki kumpopteza
hata mmoja. Upendo ni tabia ya Yesu lakini pia Yesu alikuwa na huruma Marko
6:34-44, Yesu alionyesha huruma kwa matendo na alijua kitu cha kuwafanyia wale
watu, ni kwasabau alikuwa na huruma, ishi kwa tabia ya Yesu Kristo, weka zaidi
kule kwa Bwana Yesu, pia Yesu alikuwa muombaji Luka 9:28-29, kuna muda utahitaji
kwenda mlimani kwenda kuomba. Chukua muda wa kuomba, kuwa muombaji, luka
22:39-46, Bwana Yesu pia Yesu alikuwa mpole na mnyenyekevu Yohana 8:50-54 Yesu
alimtukuza baba yake na baba yake akamuinua, ishi maisha ya kumuinua Mungu.
No comments:
Post a Comment