Mhubiri: Mch. Peter Mitimingi
Maandiko: Luka 15:20-32
kaka
ni ndugu, kaka ni mtu wa karibu, kaka ni mtu ambaye unategemea afurahie
mafanikio yako, afurahe unavyoenda mbele lakini inakuwa vibaya pale
kaka badala ya kufurahia maendeleo anaumia, kaka anaumia kwanini
umefanikiwa, kaka anatamani kuona kwamba umeishiwa. Luka 15:15-20,20-32,
inazungumziwa kuhusu habari ya mwa mpotevu, mwana mpotevu aliomba
urithi wake, baada ya kupewa urithi wake alienda nchi ya mali ktapanya
mali zake kwa anasa mpaka akaishiwa. Alipoishiwa akakumbuka nyumbani kwa
baba yake. Hapa tunapata picha mbili, moja tunamuona baba wa
mwanampotevu ambaye katika somo hili ninamfananisha na Baba Mungu.
Baba
wa mwana mpotevu anamuwazia nini mtoto wake aliporudi, Baba Mungu wa
Mbinguni anakuwazia nini wewe mwana wake. Na picha ya pili ni kaka wa
mwana mpotefu, kaka wa mwanampotevu alimuwazia nini mdogo wake aliporudi
nyumbani?
Mtazamo wa baba juu ya mwana ni nini?
Mtazamo wa baba juu ya mwana ni nini?
- Baba alimuona mwana tokea mbali, yawezekana pale kulikuwa na wafanya kazi wengi lakini hawakuona kuwa yule ni mtoto wa nyumbani kwao, macho ya baba yalimuona tokea mbali. Macho ya Mungu yanakuona tokea mbali, Mungu anakuona
- Baba alimuone huruma akampoke kwa furaha
No comments:
Post a Comment