''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 5, 2015

JINSI YA KUISHI MAISHA YA USHINDI KILA SIKU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Meshark Mhini
Maandiko: 2Wakorithno 5:4-5
 
Unaposoma Neno la Mungu ndipo unapofunguka ufahamu wako na ndipo unapofunguliwa. Sisi wakristo tunaye Roho Mtakatifu anayetuwezesha kuishi maisha ya ushindi ndio maana tunahitaji kusoma Neno la Mungu na kuomba kila siku kwa bidii, lakini usipo omba na kusoma Neno la Mungu na ukiacha kuja nyumbani mwa Mungu mapepo yatakuingia. Ni lazima uwe mwaminifu kuomba kusoma Neno la Mungu na kuja kanisani. Unaweza sema sina muda kabisa wa kusoma Neno la Mungu lakini si kweli ukidhamiria utapata hata dakika tano za kusoma Neno la Mungu na kuomba. Miaka ya tisini nilikuwa jeshini na ratiba ilikuwa imejaa yote mpaka usiku tunapangiwa vitu vya kufanya sasa nikajiuliza nitaomba sangapi lakini nkaamua ule muda wa chakula cha mchana watu wanaenda kula kwahiyo nikaamua ule muda niwe naenda kuomba tena chooni na nliuona mkono wa Mungu sana na Roho Mtakatifu alinishukia sana tangu nlivyoamua vile.
 
Usipo omba ufahamu wako utajaa vitu vichafu, Yesu awe mfano wako wa kuigwa, panga mwenyewe muda wa kuomba na kusoma Neno la Mungu ili uweze kuishinda hii dunia. Kama hautakuwa makini katika kuomba utapotea, sasa kuna kanuni za kuishi maisha ya ushindi 
 
1. Utambue kuwa ushindi ni zawadi yako kutoka kwa Mungu uanchokitaji ni kuwa karibu na Mungu na kusoma Neno lake
 
2. Hakikisha unaye Roho Mtakatifu na unamtii, ishi maisha ya utii sana,mpinge shetani nae atakukimbia, Yakobo 4:7.
 
3. Kuwa mwaminifu kwenye vipindi vyako mwenyewe vya kusoma Neno  la Mungu na kuomba pia na kushuhudia lazima upange muda wako mwenyewe wa kufanya hivyo vitu na kuwa mwaminifu katika hiyo ratiba yako.
 
4. Mungu anapendezwa na mtu anaye ishi nae kwa uaminifu na kujishughulisha 1Wathethalonike 4:1-9, Mungu hapendezwi na mtu ambaye hajishughulishi
 
5.Usifanye makubaliano au muafaka na ulimwengu wa dhambi kataa kabisa!! kabisa!!
 
6. Mtumie Roho Mtakatifu mara kwa mara ili akuongoze, mtumie muda wote Roho Mtakatifu kukuongoza katika maisha yako
 
7. Jiepushe kabisa na kukaa bila kufanya kazi au kujishughulisha, wakati wa wathehalonike walikaa tu wakasema wanamsubiri Yesu awachukue lakini Paulo akasema msipo fanya kazi na msile hata paulo alikuwa anafanya kazi ili kupata mkate wake wa kila siku, usikae bure bure, fanya kazi ili upate pato lako la kila siku, ndio Yesu anarudi lakini fanya kazi Yesu atakukuta ukiwa unafanya kazi. NI LAZIMA UISHI MAISHA MATAKATIFU YASIYO NA DOA KILA SIKU.

4 comments:

  1. Je kama nilikuwa mwizi au nilikuwa baamed au nilikuwa tapeli au namtegemea mtu ambaye aukubali wokovu na akajua naishi ndani ya wokovu nafanyaje?

    ReplyDelete
  2. Je upendo umeenda wapi wa kusaidiana na kutembeleana?

    ReplyDelete
  3. Je MTU ameokoka hana kazi anasaidiwa vipi?

    ReplyDelete