''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 18, 2015

USIUTUPE UJASIRI WAKO, KWA MAANA UNA THAWABU KUU

Mhuburi: Mzee Kiongozi, Dr. Mumghamba
Maandiko: Waebrania 10:35-39, 
 
Yesu alitolewa na Mungu mwenyewe kama tunavyoona katika Yohana 3:16, Yesu aliamua kuumia kwa ajili yetu aliteswa kwa ajili yetu.  Zamani damu ya wanyama ilikuwa inatumia kufunika dhambi za watu, kwa hiyo ilikuwa kila mwaka lazima utoe mnyama ili kufunika dhambi zako. Pia damu ya mnyama ilitumika kwenye siku ya pasaka walipaka juu ya milango na malaika aliyekuwa anaangamiza aliipita nyumba hiyo.
 
Lakini leo damu ya Yesu imetutakasa na kutuweka huru na dhambi tukaokoka, n a baada ya kuokoka tukapata ujasiri, sasa leo Mungu anatukumbusha kwamba tusiutupe ujasiri kwasababu una thawabu kuu. Lakini je ni ujasiri wa aina gani anao taka tusiuache, ukisoma Waebrania 10:19-22 "19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi."
 
Ni muhimu kufahamu hilo kwasababu ili uweze kwenda mbele za Mungu lazima uwe msafi 100% na sio 99%. Yawezekana ulianza vizuri kwa mwendo mzuri wa kumpenda Mungu lakini badae ukapunguza, mfano. ni kama mtu aliyekuja kwenye ibada kanisani alafu badae akaanza kusinzia ibadani au mtu aliye mbele za watu gafla aamue kuvua nguo kwasababu tu ya joto kali, sasa kuna watu wanapunguza ujasiri wao kwasababu ya vikwazo na majaribu wanayokutana nao.
 
Sasa ili uweze kuendelea kuwa na ujasiri lazima ufanye mambo mawili makubwa:
  1. Lazima wewe kwa hiari yako uamue kuokoka
  2. Lazima uishi maisha matakatifu yanayo mpendeza Mungu
 

No comments:

Post a Comment