''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, November 2, 2015

NGUVU YA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Meshark Mhini
Maandiko: Warumi 14:17-18, Yohana 4:14
 
Paulo alikuwa anawakumbusha watu wa rumi kuhusu Roho Mtakatifu, hata wewe leo kama huna Roho Mtakatifu amua kuwa na kiu nae, kwasababu ni wa muhimu sana, bila hii nguvu ya Roho Mtakatifu hutaweza kufanya kitu, hutaweza kushuhudia, hutapata ujasiri wa kumwambia mtu habari za Yesu, na hii nguvu ndio silaha pekee ya kushinda dhambi. utashindaje dhambi bila kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu? jibu ni huwezi.
 
Ili maisha yako yaendelee kuwa matakatifu lazima uishi na hii Nguvu ya Roho Mtakatifu lazima uitumie hii Nguvu ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anakupa nguvu ya tofauti ndani yako ambayo huwezi pata sehemu nyingine, ukiwa na Roho Mtakatifu utaweza kutoa mapepo na ukiweka mkono wako juu ya mgonjwa atapona. 
 
Ili uweze kuitunza hii nguvu lazima ni lazima ujenge tabia ya kusoma Neno la Mungu, kulitafakari na kumuomba Mungu kila siku.
 
Warumi 14:17-18 "Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu." Kama unataka amani ya kweli na furaha ya kweli kuwa na Roho Mtakatfu. Chukua muda wa kusoma Neno la Mungu/Biblia na kuomba lakini pia baada ya kusoma Neno la Mungu chukua muda wa kimya wa KULITAFAKARI Neno la Mungu. Kutafakari Neno la Mungu ni muhimu sana tafadhali tafadhali chukua muda wa kimya wa kutafakari kwasababu ukitafakari utaanza kuhisi Roho Mtakatifu akitembea ndani yako akisema na wewe ndani yako.
 
Yohana 4:14 "walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele." ukinywa maji hayo hutaona kiu tena na maji hayo ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakafitu ni Nguvu pekee ya kumpiga na kumshinda shetani, ukipoteza tu nguvu ya Roho Mtakatifu hutaweza tena kushinda dhambi.

No comments:

Post a Comment