''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, November 9, 2015

UPENDO WETU KWA YESU KRISTO

Mhubiri: Mr. Mwalongo
Maandiko: Yohana 21:1-19
 
Tunaposema upendo wetu kwa Yesu tunamuangalia Yeye mwenyewe jinsi alivyotupenda, kwahiyo upendo mkuu ni upendo wa Yesu akaacha mbingu akaja kutuokoa hivyo anastahili kabisa kupendwa na kila mmoja wetu.

Kwenye Yohana 21:1-19, hapa ni baada na Yesu kusulubishwa na kufufuka, wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekata tamaa baada ya Bwana Yesu kufa waakanza kufiikiria kurudi kwenye kazi zao za zamani kama kuvua samaki. Petro alivyowauliza wenzake kuhusu kwenda kuvua samaki wakakubali kwenda kuvua; Petro, Tomaso na wengine.

Walipoteza muelekeo wa kuendelea na kazi aliyoianzisha Bwana Yesu. Bwana Yesu alipowaona wamerudi kwenye kazi zao za zamani alisikitika sana, Yesu alitegemea kwasababu walimpenda wataendelea kufanya mambo aliyowaagiza kufanya. Baada ya kuvua samaki, Petro alipogundua kuwa ni Yesu alijitupa majini; ukipoteza upendo wako kwa Yesu utakuwa huna ujasiri wa kusimama mbele yake kwasababu hujaonyesha upendo kwa Yesu, Yesu aliyelipia thamani yako.

Baadae Yesu alimuuliza Petro, je unanipenda zaidi ya hivi (kuvua samaki, vitu vya hapa duniani) hapa kupenda sio shida unaweza kupenda kitu lakini Yesu lazima awe wa kwanza!! zaidi ya vingine vyoote. Kwahiyo swala sio kumpenda bali je unampenda ZAIDI YA VINGINE VYOTE,? swala sio kupenda ni swala la kipaombele nani unampenda zaidi, unaweza ukampenda mke wako, mume wako, mtoto wako lakin yupi unampenda zaidi???, upendo peke yake haitoshi bali Yesu anahitaji umpende zaidI ya vingine vyote umuweke kipaombele cha kwanza. Hebu jiulize Je ni kweli kabisa unampenda Yesu?? yawezekana unajipenda mwenyewe sana zaidi yake yeye, unatumia muda mwingi kwenye shughuli zako kazini lakini unampa Mungu muda mfupi. Kazini unawahami huwezi kuchelewa lakini kanisani watu wanachelewa sasa Mungu anakuuliza je unampenda kliko vitu vyote? hebu jiangalie zaidi jiulize moyoni mwako je unampenda Yesu zaidi ya kazi, watoto mwezi wako?

No comments:

Post a Comment