''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, November 15, 2015

NJAA NA KIU YA HAKI YA KUMTAFUTA MUNGU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Meshark Mhini
Maandiko: Yohana 7:32
 
Wanafunzi wake walikuwa wakiadhimisha sikukuu ya vibanda,ambapo sikukuu ya vibanda ilitokana na wana wa israeli walipokuwa safarini kwenda kaanani.
Yesu alipokwenda kuitwa naye akaadhimishe na watu wake katika sikukuu ile alisema wakati wangu bado na kuwaambia watangulie,naye baadae alikwenda kwa wakati wake, lakini katika sikukuu.

Hivyo kulikuwako na mafarisayo waliotaka kumuangamiza Bwana Yesu, Yohana 7:32. Baada ya kufika katika maadhimisho yale alianza kufundisha kama ilivyo kawaida yake,lakini mafarisayo wakaenda kinyume naye na kutaka kumuhukumu lakini falisayo mwenzao aitwae nikodemo aliwauliza swali" ni kwa nini mna mhukumu mtu kabla hamja msikiliza?" nao hawakuweza kumjibu. Nikodemo alipata hekima hii kwa kuwa alimfuata Yesu usiku na kujifunza.
 
Je,njaa na kiu ya haki inatokana na nini?
Njaa na kiu ya haki ya kumtafuta Mungu inapatikana kutokana na Imani,ambapo Yesu Kristo pekee ndiye aletaye imani inayoleta njaa na kiu ya haki ya kumtafuta Mungu. Mito ya baraka na amani itabubujika mbele zako  unapokuwa na imani iletayo njaa na kiu ya haki.
 
KWA NINI NI MUHIMU KUWA NA NJAA NA KIU YA HAKI YA KUMTAFUTA MUNGU?I. Tunatafuta uhusiano na Mungu aliyetuokoa.
ii.Tunamtafuta Bwana Yesu kwa kile tunachokiona na kushuhudia na sio kuhisi na kusikia tu.
Kanisa la leo limekuwa busy na mambo mengine kuliko mambo ya Mungu na kwa hivyo wamekosa njaa na kiu ya haki ya kumtafuta Mungu

Kuyashinda majaribu ni lazima ujawe na Neno la Mungu ndani mwako la sivyo utakuwa unapakaza rangi nje wakati ndani kuna shida. Uzima  wako wa kiroho lazima uwe na Neno la Mungu ndani yako ambapo vyote hivi hutokana na njaa na kiu ya haki ya kumtafuta Mungu. Kwa kila mmoja moja katika kanisa yampasa afike wakati ajichunguze na kurekebisha makosa yake.
 
NI KWA NAMNA IPI ITAKAYOWEZA KUKUHIMIZA NJAA HII KUENDELEA.
1.Kusoma biblia(productive bible study).upo msemo wa wazungu wanaoutumia kwamba"kama hujasoma maandiko ya Mungu asubuhi hakuna kifungua kinywa (No Bible Study No Breakfast).
2.Kutenga muda wako wa maombi pamoja na u-busy ulionao tenga hata lisaa limoja ili kuomba na kufanya maombi binafsi. Si tu kwa ajili ya maombi bali pia kwa ajili ya kutafakari. (hii ina maana kwamba usome neno la Mungu alafu unaomba, alafu mtafakari mungu) Zaburi 63:6
3.Simamia ratiba yako ya mambo hayo. Ili kufanikisha vitu hivi lazima ufanye kuwa ni tabia yako la sivyo utafanya tu mwanzo na baada ya hapo hutafanya tena. Kama danieli alivyofanya tabia yakupasa nawe pia ufanye vivyo hivyo.

 

No comments:

Post a Comment