''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Friday, January 1, 2016

TUMEVUSHWA KWA NEEMA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Meshark Mhini
Maandiko: Warumi 6:19-23, Efeso 5:15-21, 22-29, Zaburi 39:12

Ni kwa uweza wa Mungu Tu umepata uzima wa kuingia mwaka huu 2016 na sio kwa nguvu zako mwenyewe, kwasababu mwili sio mali yako roho sio mali yako chochote unachosema ni mali yako si mali yako, vitu vyote ni vya Bwana vinatoka kwa Bwana vipo kwa ajili ya Bwana kwa ajili ya utukufu wake, na ndomana tunasema tumevushwa na neema. Hata dakika chache mbele yetu hakuna anayeweza kujihakikishia kwamba ana kibali cha kuifikia. Bwana Yesu ndiye anayetupa pumzi ya uzima, nguvu. Bwana Yesu ndiye mwenye kuwezesha fahamu zetu kujua nini cha kusema, huyo ni Yesu Kristo ambaye amekuvusha kwa neema, ametushika kwa mkono wake wa kuume na kutuvusha mwaka.
 
Hebu kumbuka wana wa Israel walivyofika katika bahari ya shamu, hawakujua nini cha kufanya, wakiangalia bahari iko mbele yao na nyuma maadui wanakuja na farasi zao na silaha zao, wakaanza kumwambia Musa umetuleta huku ili tuje kuangamia lakini Mungu huyu aliyekuvusha akatoa jibu kwamba waambie wana wa Israel wasonge mbele, na Musa akapiga maji na fimbo yake, bahari ikagawanyika Mungu akawavusha salama.

 

2 comments: