''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, January 3, 2016

NGUVU YA UMOJA WA KANISA KATIKA UPENDO WA KRISTO YESU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Meshark Mhini
Maandiko: 1wakoritho 13:1-8, Yohana 17:20-26
 
Upendo wa Yesu Kristo haufananishwi na upendo wa mtu yoyote, wako wanadamu waaoonyesha tabasamu mbele yako lakini kumbe hawana upendo wa kweli. Upendo wa Kristo ni wa muhimu sana, na ili tuweze kufurika katika Roho lazima upendo wa Kristo ujae ndani yetu. Upendo wa Kristo ukijaa ndani yako hapo ndipo utamsifu na kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli.
 
Lazima utanguliwe na upendo wa Kristo, na ndio maana katika 1Wakoritho 13:1, mtu asiye na upendo wa Kristo anafananishwa na upatu uvumao. Upatu ni aina flani ya ngoma, sasa ngoma isipo wambwa vizuri haitalia kama inavyohitajika kulia, inakuwa inavuma tu.
 
Unaweza ukatenda miujiza mikubwa na maajabu na Mungu akakutumia katika hayo, lakini kama huna upendo ni kazi bure. Ukimpenda mwenzako utamsalimia, utamsikiliza mwenzako akiwa katika shida na bila baadaye kumsema, Maana kuna watu wakimsaidia mtu basi atamsema kwa watu  wengine. 
 
 Mtu mwenye upendo huvumilia, hufadhili, hana kiburi kwasababu upendo wa Kristo uko ndani yake na akifanya kinyume ya hapo Roho Mtakatifu humshuhudia kwamba hicho unacho kifanya sio sahihi. Na Roho Mtakatifu mwenyewe ndio kiini cha upendo huu.

 Basi sasa amua mwaka huu 2016 kubeba tunda la Roho la upendo na hilo ndio kusudi la Mungu kwa ajili yako. Kuwa mvumilivu mtu wa Mungu ili hata kama shida ikija usitende dhambi na kumkosa Mungu wako. Ukisemwa semwa na watu vumilia, pia katika ndoa kuwa mvumilivu; mvumilie mke wako au mume wako chukua na hata chukua muda wa kumuombea wala usiseme kwamba umemshindwa, yote yanawezekana kwa jina la Yesu. Swala la upendo ni la milele yote, katika mwaka huu chukua hili andiko liwe msingi wako. Yawezekana ofisini kwako wanakusema vibaya sasa je unawapenda?

Yohana 17:20-26 umoja katika Kristo; Haya ni maombi ya Bwana Yesu  kwamba tuwe na umoja kama wao walivyo na umoja, sasa je leo umoja katikati yetu upo? na  kama haupo  basi hayo mambo tuyaache mwaka 2015 sasa ni mwaka mpya 2016 na tuanze upya na kuwa na umoja wa kweli katika Kristo. Aliye tuokoa ni mmoja tu na huyo ndio Yesu Kristo ambaye ndiye kiunganishi chetu. Swala la umoja halipingiki, hebu jichunguze jiulize 'hivi mimi nipo kwenye kundi gani la kwenda mbinguni au la motoni?', Je una umoja wa Kristo, Je una umoja na wenzako, Je una upendo?.

Mruhusu Yesu aingie ndani yako na wewe uwe ndani yake, mkishakuwa wamoja hivyo ina maana mmeshakuwa kitu kimoja kwahiyo ukiomba maombi yako yatakwenda moja kwa moja bila vipingamizi. Muda mwingine ukiomba Mungu akiangalia ndani mwako anaona umeweka vinyongo, hujasamehe, una manung'uniko basi ukiomba maombi yanaishia hewani. Mtu anasema umesamehe lakini bado unalia sana moyoni mwako, bado una uchungu achilia watu hao moyoni mwako, ung'ang'anizi wa nini?, samehe na achilia sio ulikopwa mwaka juzi mpaka leo hii hajakulipa basi umemuweka moyoni.

Ili uweze kufanikiwa kiroho lazima utimilize masharti yafuatayo:
 1. Tambua nafasi yako kanisani,
 2. Liishi Neno la Kristo,
 3. Weka uhusiano bora na Yesu kupitia Roho Mtakatifu
 4. Enenda katika kweli, jitoe kwa Yesu, mfanye awe kipao mbele cha kwanza ili aweze kustawisha umoja.
 5. Tafuta kwa bidii kuwa na amani na watu wote
 6. Jitaidi kwa vitendo kutumikia shauri la Bwana, kama umesema unaleta nguo kwa ajili ya watu wenye shida basi fanya kweli hivyo, jitoe kwa ajili ya Yesu, Mara nyingine hubarikiwi kwasababu ya ugumu wa moyo wako, toa vitu kwa ajili ya Bwana ubarikiwe.

 Hitimisho; Mpango wako wa kila siku uombee kuwa mtu wa maombi,pia kuwa mtu unayesamehe, fanya kazi kwa bidii, jijengee ushirika na jamaa ya waaminiyo, pia utafute ufalme wa Mungu na hayo mengine utazidishiwa na la mwisho kuwa mtu mwenye shukurani, umepanga miradii mingii lakini haiendi kwasabbau hutoi fungu la kumi na Mungu hafanyi kazi na wezi. Hujatoa fungu la kumi mwaka mzima alafu unahitaji kubarikiwa?

No comments:

Post a Comment