''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, January 10, 2016

KUSIKIA NA KUITII SAUTI YA MUNGU KUNA BARAKA

Mhubiri: Mr.Fabian Masembo
Maandiko: Isaya 6:8, Kutoka 3:4

Katika isaya mtumishi wa Mungu anasema kwamba "nalisikia sauti ya bwana"hivyo kama watoto wa Mungu tuna kazi zifuatazo za kufanya:-
 
                     1.Kusikia sauti ya Mungu
                     2.kuitii sauti ya Mungu
 
Usipoitii sauti ya Bwana, Mungu atakuacha uenende mwenyewe na ukiachwa na usipokuwa na uwepo wa Mungu kinachotufuata ni balaa na laana tu. Kutoka 3:4, Mussa aliitwa na Bwana kwenda kuwachukua wana wa Israel, akaamua kuisikia sauti ya Bwana na kuitii japokuwa alijitetea kwa mambo mengi sana na hiyo ikasababisha apoteze nafasi yake ya kuwa mnenaji mkuu.

 
MIFANO YA WATU AMBAO HAWAKUITII SAUTI YA MUNGU
Mifano michache ya watu ambao walisikia sauti ya Bwana lakini hawakuitii sauti ya Bwana
  • Mwanzo 3:16-17, Adamu na Hawa walipewa maagizo kuwa wale matunda ya miti yote isipokuwa mti wa katikati ya bustani lakini hawakuitii sauti ya Mungu. Adamu na Hawa waliongea na Mungu na Kuisikia sauti yake lakini hawakuitii sauti hiyo ya Mungu. Na hiyo imeleta matatizo mpaka kizazi cha leo kwa kutoitii tu sauti ya Mungu.
  • Mwanzo 4:10-14, Hapa tunamuona kaini kwa kuenenda kinyume na sauti ya Mungu kwa kutoitii anapewa adhabu kali.
  • 2Mambo ya nyakati 18:1-34,Hapa tunaona wafalme tofauti walivyoisikia sauti ya Mungu kupitia mtumishi wa Mungu. Nabii Mikaya alisema lile ambalo Mungu alilisema na aliahidi kusema lakini mfalme hakutii na baadaye alivyoenda kwenye vita akauawa.
Mwaka huu wa 2016, Mungu atazungumza na sisi mambo mengi sana na mojawapo litakuwa habari ya kupeleka injili kwa watu wasiofikiwa, basi jitoe kikamilifu kupeleka injili kwa fedha zako na hata kwa mahudhurio yako mwenyewe kwa kwenda katika mikutano na pia wa kuwaambia watu habari za Yesu ili waokoke, maana hilo ndilo agizo letu kuu Yesu alilotuagiza wakati alipoondoka kwahiyo tulifanye kwa bidii.
 
 

No comments:

Post a Comment