''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 27, 2016

KUMJUA MUNGU NA KUMWAMINI

Mhubiri: Mr. Elisha Suku
Maandiko: Kutoka 3:1-15
 
Huu ulikuwa makutano ya kwanza ya Musa na Mungu katika kile kijiti kilichowaka moto. Katika wakati huu Musa alikuwa anamfahamu tu Mungu lakini alikuwa hajamjua kwa ndani zaidi na ishara za Mungu. Mungu alihaidi kuwaooa wana wa wana wa Israel na hapa ndipo alipoanza kutimiza kupitia Musa. Musa alikuwa anaogopa kurudi Misri kwa Farao kwasababu ya lile kosa alilofanya la kumuua mtu wa Misri. Lakini pia alikuwa anamuuliza Mungu je wana wa Israel wataniamini vipi, akamwambia awaambie ametumwa na Mungu aitwaye NIKO AMBAYE NIKO. 

 
Maana ya NIKO AMBAYE NIKO
 
  1. Kwamba NIKO yaani Mungu huyo yuko hai, Mungu yuko kikweli, je kila mtu anaamini kuwa Mungu yupo, na wengine wanajua na kuamini kuwa Mungu yupo lakini hawaamini kwamba anaweza kufanya jambo flani, . kwahiyo inatakiwa tuishi maisha ambayo yanaonyesha kwamba kweli Mungu yupo na kupitia maisha yetu watu watambue kweli Munngu yupo.
  2. Mungu habadiliki wala hatakuja kubadilika, kwahiyo inabidi au hatuja haja ya kuwa na hofu au hofu zetu zote zote tuzikabidhi kwamke . Watu wanabadilika lakini Mungu habadiliki. Kwahiyo tujifunze kumwaminni Mungu.
  3. Mungu ni mwenye nguvu sana, Mussa aliogopa kwamba akienda kule watamkamata na kumuuwa, lakini Mungu akamwambia usiogope kwasababu Bwana amesikia kilio cha watu wake na amepanga kuwaokoa, na Mussa ndio atakaye waongoza  Isaya 40:21
  4. Mungu anajua yote, kwahiyo woga wao kwamba watatokaje na itakuwaje yeye anajua jinsi atakavyo watoa. Mungu anajua mipango yote tangia mwanzo. Mungu ana mipango mizuri juu yako hata kama unaona unapita katika hali nguvu, Mungu anajua ni kwa jinsi gani atakavyokutoa katika jaribu lako.
  5. Mungu alikuwako na yupo na ataendelea kuwepo, yawezekana umekuwa na hofu kuhusu maisha unaennda huku na huku lakini mwamini Mungu kwamba YEYE YUKO AMBAYE YUKO atakusaidia atakutana na shida yako.

No comments:

Post a Comment