''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, December 11, 2016

KUWATAMBUA VIONGOZI WA KIROHO

Mhubiri: Mrs. Lucy Masembo
Maandiko: 1Thesalonike 15:12-13, Waebrania 13:17,Malaki 2:7
 
Mungu ameweka kiongozi wa kila sehemu kwa kusudi maalam.
 
Mambo 5 tunayoweza kufanya ili kutambua viongozi wetu wa kiroho:

1. KUWATII, tukiwatii viongozi wetu tutakuwa na amani sana, lakini tukiwasema vibaya viongozi wetu tutakosa amani kabisa. Tuwatii kwasababu wao ni sauti kwetu kutoka kwa Mungu, wanawasilina na Mungu wao. Kutii ni bora kuliko sadaka/dhabihu, hata kama utatoa sadaka kubwa kiasi gani lakini kama hutawatii viongozi wako wa kiroho hutaweza fanikiwa, tufanye yale maagizo wanayopewa kwa ajili yetu.

2. KUWAHESHIMU viongozi wetu. Wachungaji wanafanya kazi usiku na mchana, wanatuombea usiku na mchana wanafunga kila mara kwa ajili yako, wana kazi kubwa kwa hiyo ni vizuri kuwaheshimu. Muda wote wanajitahidi/wanahakikisha watu wote wawe na Amani. Lakini pia wanatulia usiku na mchana kutafuta chakula chetu cha kiroho, kila mara wanahakikisha watu wamepata chakula cha kiroho yani neno la Mungu. Wanakubeba katika ulimwengu wa kiroho, wanaomba Mungu akusaidie katika biashara yako, kazi yako na masomo yako. Lakini wahaishii hapo tu bali wanahakikisha tunapata chakula sahihi wanatafuta walimu wazuri na kuandaa semina kwa ajili yetu. Na sababu ya mwisho ya kwanini tuwaheshimu kwasababu wamebeba baraka zetu (Eli alimtamkia Hana kwamba mida kama ile atapata mtoto na kweli katika muda kama ule akapata mtoto).

3. KUWAOMBEA maana nao wachungaji ni wanadamu na wao wana shida kwahiyo lazima tuwaombee Mungu awatetee na kuwasaidia katika mahitaji yao katika familia zao, 2Wakoritho 1:8 "Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi". Tuwaombee wapate kibali mbele za watu na Mungu awape hekima na busara Zaidi na Zaidi.

4. KUWAPENDA, haijalishi ilimradi Mungu amemuweka katika kanisa uliopo ni lazima umpende mtumishi wa Bwana, hii ni amri na sio uamuzi wako. Mungu amewaweka makusudi kwa kusudi maalumu kwa muda maalumu, kwahiyo ni vizuri kuwapenda. 1Wakoritho 13:4-8 "4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika."

No comments:

Post a Comment