''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, July 3, 2017

NIKUMBUKE UTAKAPO PATA MEMA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Neno: Mwanzo 40:1-23

Mnyweshaji na mwokaji waliota ndoto NA HAWAKUJUA maana yake na hapo ndipo walipojuana na Yusufu. Yusufu akawaambia maana ya ndoto zao, kwamba baada ya siku tatu, mnyweshaji atarudishwa kwenye cheo chake lakini mwokaji atakatwa kichwa na kweli baada ya siku tatu yale yote yakatokea mnyweshaji akarudishwa kazini na mwokaji akauliwa.
 
Sasa ujumbe wetu unatokana na mnyweshaji (Mwnz 40:14), Yusufu alimwambia mnyweshaji kwamba yote haya yakienda sawa nikumbuke huko kwa mfalme na mnyweshaji akakubali hilo lakini tunaona mnyweshaji alivyotoka hakumkumbuka Yususfu aliyemtafsiria ndoto yake, hakukumbuka wema aliomfanyia Yusufu.
 
Sasa tunajifunza nini hapa kwanza TUSITEGEMEE WANADAMU. Usitegemee mwanadamu, mwanadamu anaweza akakuahidi vizuri kabisa lakini akakusahau, mtegemee Mungu tu. Japokuwa mnyweshaji alimkumbuka Yusufu baada ya miaka miwili na tena hapo alimukumbuka kwasababu mfalme Farao alipata ndoto ambayo watu walishindwa kuitafsiri ndipo mnyweshaji akamkumbuka Yusufu, lakini kama Farao asingeota ndoto Yusufu asingekumbukwa.

Yawezekana hata wewe umemuahidi mtu anayehitaji kitu, kuwa makini usimsahau.  Lakini pia inawezekana ulimhaidi Mungu kitu lakini ukasahau. Mara ngapi unamuomba Yesu na unamwambia ukinipa nitakufanyia hivi na hivi na Yesu anakupa kile kitu alafu unasahau kama ulimuahidi Yesu.

KAMA YOTE YAKIENDA SAWA MKUMBUKE MUNGU. unasema nikipata kazi nitakutolea mshahara wangu wote wa kwanza lakini ukipata kazi hutoi ule mshahara wako wa kwanza unaanza kupanga bajeti yako. Wengine wanamuomba Mungu awape mke mzuri na unaahidi kwamba nikipata mke mzuri nitakuja nyumbani mwako kwa furaha alafu ukipata huyo mke mzuri ndio unaanza kabisa kukosa ibadani.
 
Kwa ujumla habari hii ya Yusufu inatufundisha yafuatayo:
  • Mungu yupo tayari kutusaidia lakini tukumbuke nadhiri tulizoweka.
  • Kamwe usimtegemee Mwanadamu
  • Usiwe mnung'unikaji na kusema sema/ kulalamika katika nyumba ya Mungu. Mungu yuko tayari kukusaidia, unakumbuka ile story ya wafungwa waliosulubishwa na Yesu, mmoja alianza kumlalamikia Yesu kwanini usijiokoe mwenyewe lakini mwingine alikubali kwamba yeye ni muovu lakini Yesu hajafanya kitu na akamuomba amkumbuke katika ufalme wake
  • Unaweza ukahukumiwa kwa bahati mbaya kwenda gerezani lakini kumbuka kwamba kuna tumaini, Mungu atakukumbuka tu. Huna kazi? Mungu atakukumbuka atakupa kazi, huna mke/mume Mungu atakupa mke/mume, Mungu atakupa kiwanja.
  • Yusufu hakulipiza kisasi kwa mnyweshaji baada ya kutoka bali alitafsiri ndoto ya mfalme vizuri bila tatizo, usiwe mtu wa kulipiza kisasi.
 

 
 

No comments:

Post a Comment