''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 23, 2017

TAFUTA MAJIBU KWA KRISTO YESU

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Maandiko: 2Wafalme 1:1-17, Mathayo 18:18-20


Mfalme Ahabu alipougua alitafuta majibu juu ya uponyaji wake kwa wanadamu badala ya kwa Mungu, wala hakupata majibu kuhusu uponyaji huo. Wakiwa katika kutafuta majibu malaika wa Bwana akamtokea nabii Elia na kumwambia akawarudishe wajumbe wa mfalme, warudi kwa mfalme Ahabu, wakamwambie kuwa atakufa na wala hatapona.

Mfalme Ahabu akataka kumjua ni nani mtu huyo aliyemwambia hivyo na yukoje, baada ya maelezo akatambua kuwa ni mtumishi wa Mungu Elia. Lakini, badala ya kutubu mbele za Mungu, akatuma akida na askari Hamsini wamkamate Elia na wampeleke kwa mfalme. 

Eliya nae akashusha moto ukawateketeza akida na askari wake hamsini, habari zikamfikia mfalme. Lakini Mfalme hakuelewa kuwa kafanya kosa wala hakujishusha wala kutubu akatuma tena kikosi kingine kwa Elia kikateketezwa kwa moto tena, mpaka kikosi cha tatu ambacho akida alinyenyekea na kumsihi Elia, ndipo Elia akakubali kushuka.

Ziko mamlaka za kawaida lakini ipo mamlaka kuu kuliko zote ambayo ni mamlaka ya Ki-Mungu. Kanisa la Mungu Ndio Mamlaka ya Ki-Mungu hapa Duniani. Mfalme Ahabu baada ya kutambua uwepo wa Mtumishi wa Mungu Elia hakupaswa kutangatanga kutafuta majibu ya uponyaji wake kwa miungu ya Misri. 

Mpendwa katika Kristo sisi kama watumishi wa Mungu yatupasa kutafuta majibu yetu kwa Yesu Kristo. Yesu Kristo pekee ndio mwenye uwezo wa kutatua shida yako. Na si kila huduma inayoonekana kuhubiri injili inamhubiri Yesu huyu huyu aliyetuokoa. 

Tafuta majibu yako kwa Yesu Kristo tu!.

Kanuni ya kupokea kwa Mungu ni kuomba lakini kwa yale mambo yaliyo ndani ya mapenzi yake, omba kitu ambacho ndani yake kina mapenzi ya Mungu, utatambua mapenzi ya Mungu kwa kusoma Neno lake.

No comments:

Post a Comment