''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 30, 2017

KUWAFIKIA WENGINE

Mhubiri: Mr. Leandri Kinabo
Maandiko: Matendo 16:9-15

Paulo na Sila waliongozwa na Roho Mtakatifu kwenda Makedoni ili kuwafikia watu wa mji ule uliokuwa unakuwa kwa kasi na watu wengi zaidi wakiongezeka. Ni vizuri sana kuongozwa na Roho Mtakatifu, na ni vizuri sana kuwa na mawasiliano mazuri na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anakupa nguvu ya Mungu katika maisha yako. Kwahiyo ni muhimu sana kuwa na Roho Mtakatifu.

Mambo ya muhimu ya kujua kuhusiana na kuwafikia watu wengine:

1. Ni lazima uwe maisha ya maombi, maombi ni ya muhimu sana kabla ya kuwapelekea wengine Neno la Mungu. Maombi yatakupa nguvu mwenyewe na kukufanya uwe tayari kwa kazi iliyo mbele yako.

2. Chukua Hatua, ni lazima ukubali kuchukua hatua ya kwenda, usikae nyumbani tu. Hatua inatakiwa, tumeambiwa tutoke tukashuhudie sasa usikae tu nyumbani, ukianza kwenda kushuhudia Yesu atakuongoza nani wa kumshuudia.

3. Mungu atakupa mahitaji yako. Matendo 16:15, unaona Paulo walifanya kazi ya Bwana na Bwana akaanda mtu wa kuwajali katika mji ule mpya kwao, akawapa sehemu ya kulala. Kuna faida kubwa sana ya kumtumikia Mungu. Unapofanya kazi ya Mungu, Mungu pia anafanya kwako pia zaidi. 

4. Kumtumikia Mungu hakuhitaji pesa bali kinacho hitajika ni utayari wako; 
2Kor 8:1-5, watu wa Makedonia walikuwa ni watu masikini lakini utayari wao ukawafanya wamtolee Mungu.

5. Furaha ya kweli utaipata ukimtegemea Mungu TU. Kama unahitaji furaha ya kweli ni lazima umtegemee Mungu kwenye kila kitu chako na hali yoyote utakayo pitia. 
2Kor 8:2 ukifanya kazi ya Mungu haijalishi ni masikini au tajiri Mungu atakupa furaha ya kweli.

Tumeitwa kufanya kazi ya kuwaambia watu habari njema ya Mungu! 
Mathayo 28:18-20

No comments:

Post a Comment