''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, August 7, 2017

KANUNI ZA KUMFUATA YESU

Mhubiri: Mch. Emmanuel Sote
Maandiko: Luka 9:23


Kuna watu wanadhani wanamfuata Yesu lakini kumbe wanamkana Yesu katika Maisha Yao.
Kuna shida katika ufuasi na ndio maana kuna vituko vingi makanisani. Si wote wanaosema wanamfuata Yesu basi watamfuata Yesu, wengine watamkana Yesu. Anayetaka kumfuata
Yesu anapaswa kujikana nafsi yake, ni lazima uikane nafsi yako kwasababu kwa asili ya nafsi huwa ina tabia ya kuusikiliza mwili nini unataka badala ya kusikiliza nini roho inataka. Ndio maana rohoni mwako unaweza ukajisikia kutenda mema lakini ukajikuta unatenda dhambi kwasababu nafsi yako ambayo hujaikana. 

Luka 6:46
Yesu akiwa anatembea na wanafunzi wake aligundua kuwa kuna watu ambao pamoja na kuwaelekeza mambo ya ufalme wake bado walikuwa wazito kuelewa.
Yesu anawaambia "kwa nini huniita Bwana Bwana lakini hamtendi nayowaambia?"
yaani kwa nini mnanifuata mimi lakini hamfanyi yawapasayo kufanya.

Tatizo katika ufuasi ni la kutofanya yale yatupasayo kufanya. Yatupasa kufuata kanuni za ufuasi na wala si kuwa wafuasi kwa kanuni zetu binafsi.

KANUNI
1. Lazima utake mwenyewe
Usiangalie watu bali amua wewe mwenyewe kumfuata Yesu na ukawe mfuasi wa Yesu Kwelikweli.

2. Lazima Ujikane Nafsi Yako Mwenyewe
Kuishi nje ya matakwa yako mwenyewe na badala yake uanze kuishi kwa matakwa ya Mungu. Lazima uiambie nafsi yako kwamba wewe ni wa rohoni hivyo mambo ya dunia na matendo ya dunia hayana nafasi kwako.

3. Lazima ujitwike msalaba wako kila siku
Kama ulilazimishwa kuokoka huwezi ukabeba msalaba wako mwenyewe maana hukua na dhamira ya kweli juu ya kuwa mfuasi wa Mungu, lakini kama hukulazimishwa utakuwa tayari kumng'ang'ania Yesu wala hutajali magumu utakayopitia. Msalaba ni mateso, na Yesu akasema wazi kabisa kwamba mtu ambaye hajajitwika msalaba wake na akataka kumfuata Yesu huyo hamfai.

No comments:

Post a Comment