''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, August 14, 2017

KUBALI WITO WAKO MKUU!

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Yona 1:1-3,4-16

Kila mmoja wetu ana jukumu lake la kwanini ameumbwa, haukuletwa tu dunia hivi hivi kila mtu ana kazi yake maalumu katika mwili wa Kristo. Ili ujue kazi yako ni nini, ni lazima uwe na tabia ya unyenyekevu na kumsikiliza Mungu.

Tunaona Yona alitumwa katika mji wa Ninawi lakini alikataa wito ule, akaenda Tarshishi mahali ambapo hakutumwa. Alikuwa anakimbia wito alioitiwa na Mungu, hili lilimkasirisha Mungu. 

Yona yupo kama baadhi yetu ambao wameitwa wamepewa kazi na Mungu lakini wanakimbia ile kazi au wanajuka tu kanisani lakini hawafanyi ile kazi aliyopewa na Mungu.
Kila mtu ana wito wake maalum na kama mtu mwenye Roho Mtakatifu utakuwa unajua kabisa kazi yako, lakini kwanini unakimbilia tarshishi?. Yona alikataa kwasababu tu hakutaka kufanya kazi ya Mungu, unajua wito wako kabisa alafu hufanyi. Yona alipewa adhabu ya kumezwa na samaki. Yona 2:10, unapotumwa au ukijua wito wako alafu hufanyi ni hakika utapata adhabu!.

Yona 1:4-16 tunaona madhara ya kutosikiliza au kufanya kile Mungu alichokutuma, Yona alimezwa na samaki siku tatu kisa hakwenda alikotumwa. Sasa wewe ni mtumishi wa Mungu fanya kile kitu ulichotumwa na Mungu kabla hujapewa adhabu, usiwe kama Yona, kama Roho anakuagiza ufanye kitu, basi fanya kama Mungu aivyokutuma, usisubiri kumezwa, kwahiyo jifunze kutoka kwa Yona. Unapopata wito kwa Mungu fanya wito ule ule usijibadilishie wala kuukimbia.

Warumi 12:6-8, karama ziko nyingi sana, kama wewe wito wako ni mtoaji basi toa kwa uaminifu, kila mtu ana kitu alichopewa na Mungu, basi kifanyie kazi kwa uaminifu. Katika kanisa la Mungu kuna mengi sana ya kufanya hakuna kitu kidogo hata kama wewe unajisikia kupamba kanisa fanya hicho kwa uaminifu, kama wewe ni mwalimu au unasijikia kufundisha sunday school waambie viongozi utapewa nafasi. Mungu anakuita sasa kufanyia kazi kitu alichokuitia. Muombe Mungu msamaha kwa kutofanya kazi/wito wako, Mungu yuko tayari kukusamehe na kukusaidia kufanya wito wako.

No comments:

Post a Comment