''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Friday, September 8, 2017

MSAMAHA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Mathayo 18:21-22

Msamaha ni tendo la muhimu sana, kama unataka ujibiwe maombi yako ni lazima usamehe, bila kusamehe Mungu hatakusikia. Kutokusamehe ni tatizo kubwa sana. Ndio kuna marafiki, ndugu zako wanaokuuzi lakini Yesu amekuagiza usamehe, kushindwa kufanya hivyo ni kinyume ya matakwa yake.

Dhambi ilipoingia duniani Mungu aliweka utaratibi kwamba ukimuomba msahama kwa kumaanisha Yeye atakusamehe, kwahiyo wewe uliyeokoka ni zao la kusamehewa. Tendo la kusamehe ni la muhimu sana katika maisha yetu, wewe kama mtu unayempenda Mungu alafu ukashindwa kusamehe basi ujue huna Mungu wa kweli maana Mungu wa kweli lazima akupe uwezo wa kusamehe.

Mathayo 6:14-15, kama hutasamehe na Mungu hatakusamehe. Wewe kama mwanadamu pia hujakamilika unakwaza na kuuzi wengine 1Yohana 1:8-9 kwahiyo unaweza ukatenda dhambi sasa ni muhimu kujua kuomba msamaha na kusamehe. Hata kama wewe ni mkubwa kuna muda unamkosa mdogo, wewe ni mzazi kuna muda mwingine unamkosa mtoto wako muombe msamaha. Kama ndani yako bado hujamsamehe mtu bado una kinyongo nae, utaomba na kuomba miaka na miaka maombi yako hayatajibiwa mpaka ukubaki kumsamehe. 

Matendo 13:38 Yesu huyu tunayemuongelea hapa ni mfano namba moja wa kusamehe wengine, kupitia Yesu dhambi zetu zimesamehewa, ni kwa kupitia Yesu tu ndio tunapokea msamaha. 

Ukisamehe watu waliokutendea mabaya unaweka uhusiano wako mzuri na Mungu wako. Usiweke uchungu ndani mwako, uchungu ni kitu kabaya mno, uchungu unatengeneza kitu kibaya ndani mwako inaweza sababisha magonjwa ya msongo wa mawazo. Uchungu ni sumu mbaya sana kwa maisha ya mkristo, samehe mume/mke wako, rafiki yako, jirani yako. 

No comments:

Post a Comment