''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 10, 2017

TATHIMINI MAISHA YAKO, JIWEKE SAFI!

Mhubiri: Mch. Mussa Eliasi
Maandiko: 1Wathethalonike 5:23-24

Katika huu mstari kuna neno la muhimu, kutakaswa. Ni kawaida ya binadamu wote kujiweka safi kujisafisha vizuri ili kukutana na mtu maalumu, kwahiyo kutembelea au kutembelewa huwa inafanya mtu afanye usafi mzuri. 

Kutakaswa kuna maanisha kusafishwa vizuri mpaka uwe safi kabisa. Kwahiyo na wewe kama mtu unayetegemea kwenda mbinguni, unatakiwa uwe msafi maana Yesu atakuja muda wowote. 

Mungu anafanya kazi na watu watakatifu. Yesu yu karibu kurudi, anataka uwe msafi sio roho yako tu bali roho, nafsi na mwili wako. Binadamu ana sehemu tatu (3) maalum; roho nafsi na mwili. Leo Mungu anakukumbusha kuwa safi kwanzia mwili wako.

Kitu unachojaza ufahamu wako ndicho kitakachotoka, ukijaza uchafu utashangaa mwenyewe vitu vitakavyotoka, kuwa makini sana na nini unajaza kwenye ufahamu wako ambayo ni sehemu ya nafsi. Mwili unaongozwa roho na nafsi, roho ni kama 'engine' alafu nafsi ni 'transmission system'. Unavyojaza vitu sahihi kwenye fahamu zako unakuwa hata na ujasiri mbele za watu, kama umejaza uchafu huwezi kuwa na ujasiri.

Yesu anakuja lakini ataondoka na watu walioosha nguo zao tu, si za mwilini bali za rohoni, tena walioosha mara kwa mara, kumbuka kutubu kila wakati. Hivi unaruhusu vipi kufanya mazungumzo ambayo unajua kabisa hayampendezi Mungu?, unatembeaje au unaundaje urafiki na mtu ambaye unajua kabisa hana mambo ya Mungu? au atakupunguzia uwepo wa Mungu ndani mwako?, kwanini unaruhusu vitu kama hivyo?, acha kufanya hivyo. Kila siku jitathimini maisha yako mwenyewe je unajiona uko safi au mchafu? tubu kila siku.

No comments:

Post a Comment