Mhubiri: Elisha Suku
Maandiko: 1korintho 1:18-24
Neno la msalaba kwa wanaopoteza ni upuuzi lakini kwa sisi tulio kwa Yesu ni nguvu ya Mungu. Kwa wasiomjua Mungu ni upuuzi kwasababu hawaelewi kilichofanyika, Wayahudi walikuwa wanatafuta hekima kutoka kwenye habari ya kuja Yesu walikuwa wanatumia akili zao binafsi ndomana hawakuelewa kabisa wala kuamini kama kweli Mesaya/Kristo waliokuwa wanamtarajia atatundikwaje msalabani? kwahiyo hawakuona mantiki hapo ndomana kwao ilikuwa ni upuuzi kumbe ile ndio ukumbozi wetu.
ISAYA 53:1-10, Nabii Isaya alitabiri mateso ya Yesu. Yesu alipata mateso makali sana lakini hakusema kitu, mstari 4 alichukua mateso/masikitiko yetu, kwahiyo ndomana tunasema ni nguvu yetu maana alichukua mateso yetu lakini watu wa nje hawaelewi. Mstari 5: mateso yake yalituletea amani aliteswa sana, muda wote yapaswa kumsikiliza Yesu.
COLOSAI 2:13-15, Tunakumbushwa tulikuwa tumekufa kwasababu ya maovu yetu dhambi zetu, Yesu akaja kutuokoa akatufanya kuwa hai, na kwendana na sheria na asili ya dhambi kila mmoja wetu alikuwa na kosa na bila Yesu kamwe tusingeweza kujiokoa. Sasa Yesu alichokifanya ile hukumu yetu ambayo tusingeiweza akaichukua na kuigongelea msalabani na kuhairisha makosa yote, na sio hivyo tu lakini pia (mstari 15)alizima kila silaha za shetani
Kwahiyo sasa tufanyaje? GAL 5:24, tunatakiwa kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu, Mungu ameshatuokoa na amefuta makosa yetu yote, Yesu hakufa bure, kwahyo tunatakiwa tufanye mapenzi yake. PIA MATH 16:24-25, Tunatakiwa kujikana wenyewe na kuacha dhambi zotee usikubali madhahifu tenaa.
No comments:
Post a Comment