''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 24, 2017

ONDOA MIUNGU YA KIGENI KWANZA

Mhubiri: Steven Wambura
Maandiko: 1Samwel 4:1-10,1Samwel 7:3-14, 2Wakorintho 9:10

Wazee wa Israeli walikuwa wakipigwa na wafilisti mara kadhaa nao wakakaa chini na kujiuliza swali kwamba, "kwa nini tunapigwa?", Swali hili ndio latupasa kujiuliza katika kumtumikia Mungu wetu. Wewe umeokoka ni mtoto wa Mungu lakini kwanini mambo hayaendi? kila siku uko palepale hauna maendeleo unayotamani.

Mungu hutuwekea vitu mbele yetu ili tunapofanya sawa sawa na makusudi yake apate kutubariki. Katika 1 sam 7:3 na kuendelea jibu la swali walilokuwa wakijiuliza wale wazee wa Israeli "kwa nini tunapigwa".Jawabu lilikuwa katikati ya wana Israeli kulikuwa na miungu iliyo ya kigeni. 

 Mungu hachanganyi na kingine, anataka umtegemee Yeye tu. Ondoa miungu ya migeni ndani yako, ili Mungu atembee na wewe. Amua upya na ufanye toba ya kweli.
  
  

No comments:

Post a Comment