''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 21, 2018

HURUMA YA MUNGU KWA WAHITAJI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Isaya 54:11-17

Mpango mkuu wa Mungu ni kuwaweka huru wanadamu, na hili ndo kusidi lake kubwa, na matatizo yanapokuja huwa anaonyesha kuwa ni Yeye tu ndiye anayeweza kukusaidia. Mungu hachagui mtu kwa rangi yake wala hana ubaguzi wowote bali anasaidia mtu yoyote atakaye nyenyekea mbele zake, kumwamini Yeye na kuhitaji msaada wake. Kwahiyo ni kweli majaribu yatakuja lakini ni mmoja tu ambaye atakusaidia jaribu lako au shida yako, ni yeye tu anayeweza kuelewa kwa uhakika jinsi unavyosikia au maumivu unayopitia katika hali uliyopo, na huyo ni Yesu Kristo. 

Unakumbuka Yesu aliona watu wana njaa akawaonea huruma akaombea mikate ikawalisha maelfu. Yesu ni mwenye huruma sana. Kwahiyo ukiwa kwenye shida usiseme kwamba Mungu amenisahau bali endelea kwenda kwa Mungu mwenye huruma, kwa kumuomba na atakujibu kwa wakati sahihi.

Ukisoma zab 9:18, tunaona Mungu kamwe hamsahau mwenye uhitaji, bali unachohitaji ni umwendee Mungu kwa kumaanisha, Mungu hawezi kukusahau. Zab 25:3 maaadui zako wataaibishwa, kwahiyo usiogope Mungu yuko upande wako, cha kufanya wewe ni kukaa na Yesu vizuri kwa kusoma sana Neno lake na kuomba kwa bidii naye Yesu atakuonekania, na kukuonyesha njia ya kuelekea. Zab 107:41 atakuweka juu mbali na mateso. Isa 49:14-15 kuna ahadi kwamba Mungu hawezi kukusahau, mmama anaweza kusahau mtoto wake lakini sio Mungu, hata kama unapitia changamoto kubwa sana Mungu hajakusahahu endelea kuomba Mungu atakujibu tu. 

No comments:

Post a Comment