Mhubiri: Mch.Kiongozi, Abdiel Meshark Mhini
Maandiko: Matendo 6:8-11, 7:54-60
Hizi ni habari za Stefano, aliyekuwa ni mtumishi wa Mungu. Stefano alikuwa amejaa Roho wa Mungu, alitangaza habari za Yesu kwa nguvu sana na kuwaambia watu kweli ya Kristo lakini watu wa sinagogi wakamchukia na kuamua kumpiga kwa mawe. Stefano alipigwa sana lakini hakusema baya kwao.
Sasa tunajifunza nini hapa?
Stefano alikuwa na uhusiano mzuri na Mungu, ndomana alikuwa akitangaza kweli yake Mungu kwa bidii yote. Stefano alikuwa amejaa Roho Mtakatifu muda wote ndio maana maneno yake yalikuwa ni ya hekima kubwa sana akawashinda wale waliomshitaki wakaamua tu kumsingizia uongo. Lakini pia Roho Mtakatifu ndani yake alimfanya awe na ujasiri sana na uhodari wa kulitangaza Neno la Mungu.
Amua leo kuwa pamoja na Mungu kwa kumaanisha, amua kuwa na Roho Mtakatifu muda wote, usiwe kama wale watu ambao wanakuwa karibu na Mungu akiwa kanisani tu akitoka kanisani anakuwa kama kamuacha Mungu, au siku ya jumapili tu ndo anakuwa mtakatifu alafu siku nyingine anakuwa sio mtakatifu.
Na hapa pia tunaona Stefano alikuwa ni hodari wa imani na Yesu alikuwa tayari kupokea roho yake. Alikuwa na uhakika 100% na Mungu wake na akaamua kama wataniua kwa ajili ya Mungu na waniue tu. Huu ni mfano mzuri wa mwanafunzi mzuri wa Yesu, Je wewe ni mwanafunzi mzuri?? Je umejipangaje mwaka huu kuwa mwanafunzi mwaminifu? Kuwa pamoja na Yesu? Je uko tayari hata kufa kwa ajili ya Yesu?. Umejipangaje kulitangaza jina la Yesu?, unampango wa kushuhudia? ni kwa kiasi gani basi umejipanga?.
Unajua hawa watu waliokuwa wanampiga stefano hawakufanikiwa lengo lao, kwanini? Kwasababu Stefano alikuwa pamoja na Yesu, hawakusababisha amuache Yesu.
Stefano ni mfano mzuri kwetu, kuokoka tu haimaanishi kwamba ndo umemaliza sasa upumzike hapana hiyo ni hatua tu ya kwanza ya kumkubali Yesu kwahiyo baada ya kuokoka lazima ukasashirikishe wengne habari za Yesu. Matendo 1:8, ni lazima uwe na Roho Mtakatifu ili uweze kushuhudia.
No comments:
Post a Comment