Mhubiri: Mch. Kngz. Abdiel Mhini
Maandiko: Joshua 24:14 -27, Waamuzi 2:11-19, 1Kor 10:14-17
Joshua aliwauliza wana wa Israel ni Mungu yupi watakae mtumikia kwasababu aliona wamerudi nyuma na kugeukia miungu ya kigeni, akawakumbusha jinsi Mungu alivyowatoa Misri kwa matendo makuu. Katika kipindi hicho wana wa Israel walikuwa wanaonywa mara kwa mara lakini wanarudi nyuma, wanamshika Mungu kwa muda kidogo alafu wanarudia miungu ya kigeni; kwahiyo hapa akataka waamue wenyewe ni Mungu gani watamtumikia.
Waamuzi 2:11-19, tunaona wana Israel walikuwa wamebadilika sana, walikuwa dhaifu sana katika kumfuata Mungu, kila wakati anapokuwa mwamuzi na wao wanarudi kumtumikia Mungu, mwamuzi akiondoka basi wao wanarudi nyuma sana kuliko hata mwanzo walivyokuwa. Tatizo lao kubwa lilikuwa ni kujichanganya na mataifa na kuabudu miungu ya kigeni. Usiache kuifuata sheria, Yesu hakuja kuitangua sheria bali kuitimiliza.
Joshua anawakumbusha wampende Mungu wa kweli na kuwa waaminifu kwake. Je wewe ni mwaminifu kwa Mungu?, je unatii maagizo ya Mungu? Joshua awe mfano wa kuigwa kwetu. Wengine wenu mmeshasahau ibada za katikati hauhudhurii ibada ya jumatano, ijumaa, na mkesha hata kama una muda. Acha hiyo tabia badilika leo, acha kupuuzia maagizo, mara nyingi kanisani maombi hutangazwa lakini ni mara ngapi unahudhuria?
Acha kujichanganya na mataifa acha kuishi kama mmataifa, wewe umeamua kuokoka basi mtumikie Mungu kwa moyo wote. Muda umefika wa kujikagua mwenyewe kama je ni Kweli unamtumikia Mungu kwa uaminifu?
No comments:
Post a Comment