''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, March 25, 2018

JITAMBUE KUWA WEWE NI WA TOFAUTI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: 1Petro 2:9-12

Je wajua kuwa wewe ni mtu wa tofauti, tofauti na wamataifa. Ni kwasababu  umeoshwa kwa damu ya Yesu, kwahiyo hutakiwi tena kutamani mambo ya dunia hii. Jielewe kuwa Wewe umechaguliwa na Mungu, Mungu, na kama umechaguliwa na Mungu ufahamu kwamba wewe una ruhusa ya kumuomba Mungu moja kwa moja. 

Na wewe kama mtu wa Mungu ni lazima ujue kwamba hutakiwi kuishi kama mtu wa mataifa, huna hata muda  wa kuomba na kusoma Neno, jitambue kwamba wewe ni wa tofauti sio kama mmataifa usiombe kwa muda mchache tu inatakiwa hata lisaa, wewe ni kuhani hakuna kuhani asiyeomba ni lazima uombe., 2Nyakat 7:14-15 Mungu atasikia, wewe kama mtu wa Mungu ukiomba Mungu atasikia kutoka mbinguni, mstari 15 anasem masikio yake yatasikia, macho yake yataona. 

No comments:

Post a Comment