''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, April 1, 2018

NGUVU YA UFUFUO

Mhubiri: Dr. Elifuraha Mumghamba
Maandiko: Luka 24:1-12, 36-49

Yesu kabla hajasulubiwa aliwaambia wanafunzi wake kuwa siku ya 3 atafufuka lakini  wanafunzi wake hawakuamini inatokeaje mtu kukufufuka, wasijue kuwa Mungu ana uwezo mpaka wa kufufua. Kama Yesu asingalifufuka hata leo watu tuliookoka tusingekuwa na la kujisifu lakini Yesu kafufuka tumewekwa huru tuna haki ya kujisifu kwa ajili ya Yesu. Kuna nguvu ya ufufuo ndani ya Jina la Yesu.

Katika Biblia kuna miujiza 10 ya ufufuo, mmojawapo ni Yesu alipomfufua Lazaro baada ya kuwa kaburini kwa siku 4, alikuwa ameshaanza mpaka kutoa harufu lakini nguvu ya ufufuo ikamrudisha tena akawa hai. Nguvu hii ya Mungu ni kubwa mno, ukiiamini yaweza kufufua mipango yako/ mambo yako yaliokufa siku nyingi yakahuishwa na kuwa hai tena, mwamini Mungu tu anaweza yote.

Ndio Yesu amefufuka, lakini je unaijua nguvu ya ufufuo? Paulo kwenye wafilipi 3:9-11 anasisitiza tumjue Yesu na uweza wa kufuka Waaflme 13:20-21,Dorcas alifufuliwa na Petro, isaya 57:15 nguvu ya ufufuo inaamsha vile vilivyolala, watu weng sasa wamepoa kiroho lkn nguvu ya ufufuo itakuamsha tena.


No comments:

Post a Comment