''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 8, 2018

UNAHITAJI MACHO YA KIROHO

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Luka 24:13-32

Watu hawa walikuwa wakitembea kwenda Emau umbali wa kilometa 11.26 (7 miles), Yesu akajiunga nao lakini kwasababu hawakuwa na macho ya rohoni hawakujua kama ni Yesu. Kileopa akashangaa huyu ni mgeni Yerusalemu hajui yaliyotokea na akamuhadithia kisa chote asitambue uwa anaongea na mhusika mwenyewe. 

Walitembea nae Yesu umbali mkubwa hivyo lakini wala hawakutambua, ili kuona mambo mengine ni lazima uwe na macho ya kiroho. Ni lazima uwe na macho ya kiroho ili kujua mambo ya kiroho yanaenda vip. Huwezi kujua nini kinaendelea kama huoni rohoni, na ili uwe na nguvu ya kuona ni lazima uwe na tabia ya kusoma Neno la Mungu sana na kuomba kwa kumaanisha.  

Lazima uamue kusoma Neno la Mungu na kuomba na kutafakari, unaposoma Neno kwa kumaanisha alafu ukalitafakari vizr na ukaomba hapo ndipo utakapopata nguvu ya kiroho na kuona katika roho. 

Jiulize Je ndani yako himu una roho mtakatifu. Wakati wa sasa wakristo wamejichnganya sana na mambo ya kidunia na ndiomana hawawez kuona macho yao yamewekwa giza. Acha kuizoea dhambi, rudi kwa Bwana naye atakusamehe.

No comments:

Post a Comment