Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Yakobo 2:22-26
Kusema umeokoka peke yake haitoshi, kitakacho thibitisha ni matendo yako. Matendo yako yataonyesha kweli wewe ni mtu mfuasi wa Yesu Kristo au lah. Ndio umepokea wokovu kwa njia ya imani, lakini imani bila matendo haifanyi kazi.
Imani na matendo vinafanya kazi pamoja, Imani inakamilishwa na matendo. WaKristo wengi wa sasa ni wasikilizaji wa Neno lakini sio watendaji, wanalijua Neno la Mungu lakini hawaliishi, wanaokoka lakini hawaishi maisha ya wokovu. Amua leo kumfuata Yesu na kufanya matendo yanayompendeza Yesu.
Ni lazima ulitendee kazi Neno la Mungu kama linavyokuelekeza, Umeamua kumfuata Yesu basi litendee kazi Neno lake, maagizo yake aliyotuachia. Kusikia Neno la Mungu alafu usilitekeleze kama linavyokuongoza ni sawa sawa na sifuri. Ni vizuri ukakubali kulitendea kazi Neno la Mungu, ukakubali kuliiishi Neno la Mungu ili uweze kuwa mtakatifu ili Yesu atakapo rudi uweze kwenda naye.
No comments:
Post a Comment