''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 10, 2019

AMANI NA ULINZI WA MUNGU

Mhubiri: Mch. Kiongozi. Abdiel M. Mhini
Maandiko: Yeremia 33:1-9

Amani itokayo kwa Mungu ni ya pekee sana, katika maisha tunapitia majaribu mengi lakini katika hayo yote Mungu analeta amani na ulinzi wake. Mungu atakupa furaha tena na kukuweka huru mbali na vifungo vya kila hali. Mungu aliwatangazia wana wa Israel Uhuru wao baada ya utumwa wa muda mrefu sana, Mungu aliwakumbuka na kuwasamehe walipomrudia.

Mungu yuko tayari kukusamehe dhambi zako kama ukitubu, haijalishi ni dhambi kiasi gani Yesu yupo tayari kukusamehe na kukuweka huru tena kukutoa katika utumwa wa shetani. Kwanini yuko tayari kukusamehe? kwasababu Yesu ana Upendo wa Kweli Kwako, hivyo hivyo ulivyo Yesu anakupenda sana. Yesu anakuhurumia yuko tayari kukutoa kwenye vifungo. Japokuwa Wana wa Israeli walimtenda Mungu dhambi lakini Mungu alikuwa yuko tayari kuwasamehe na aliwasamehe. 

Ili upate hii amani na ulinzi ni lazima ufanye yafwatayo:
1. Jiweke mwenyew katika Imani ya kweli na umkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako Warumi 5:1-12, hiyo shida uliyonayo ni kwasababu umetoka nje ya mpango wa Mungu. Ni lazima utulize ufahamu wako kwa Yesu na utembee na Roho Mtakatifu.

2. Tembea kwa utiifu katika Sheria zake, Mhubiri 26:3-6. Utakapo tii sheria za Mungu utapata amani kwenye maisha yako, kwenye ndoa yako.

3. Weka Neno la Mungu kwenye matendo. Unaposoma Neno la Mungu au kusikiliza mahubiri kama hutayaweka katika matendo hutapata faida; Wafilipi 4:9

4. Kuwa muombaji na mtu mwenye kumshukuru Mungu. 

No comments:

Post a Comment