''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 17, 2019

UTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: 1Petro 1:2-5

JE MTAKATIFU NI NANI? Kuanzia mstari  wa pili unajibu swali hili, MTAKATIFU ni yule anayetafuta na kutunza uhusiano wa karibu na Yesu Kristo katika kila siku ya maisha yake. Mtu huyo anakuwa ni makini kuhusu sana na Mungu wake, anakuwa mwenye bidii ya kusoma Neno la Mungu na kuomba. Sasa hebu jiulize je unasifa hizo za mtakatifu?, Jikague mwenyewe, je uhusiano wako na Mungu uko vizuri?, kama hauko vizuri na Mungu basi amua leo kutengeneza.

Ili Uendelee Kuwa Mtakatifu ni Lazima Uyazingatie Yafwatayo:

1. Yoh 17:15-16 "Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu".  Ni lazima ukumbuke kuwa wewe si wa ulimwengu huu.

2. Yakobo 4:4 "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu". Acha kabisa kuwa rafiki wa hii dunia, na unaweza kuwa rafiki wa hii dunia kwa njia nyingi hata kuangalia tamthilia ambazo hazimpendezi Mungu, kusikiliza miziki isiyo ya Mungu.

3. Efeso 6:10-12, "Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho". Ili kuendelea kuwa mtakatifi ni lazima uvae silaha zote uli uweze kumshinda shetani, na ni lazima uende kinyume na kila nguvu inayoenda kinyuma na Mungu, ikemee kabisa!, shetani anakuwinda kila wakati kwahyo ni lazima uwe makini.

1Yoh 1:6, "Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli". Unaposema umeokoka alafu unaendelea kufanya mambo ya kidunia hapo unajidanganya, wewe jitambue kwamba sahivi nimeokoka ni lazima ufuate maagizo ya Mungu kutoka kwenye Biblia, acha kabisa mambo ya kidunia, mienendo yako lazima iwe tofauti.

No comments:

Post a Comment