''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 24, 2019

ALILOKUAMBIA YESU LIKAMATE

Mhubiri: Mrs. Masembo
Maandiko: Marko 4:35-41

Marko 4:35-41 "35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. 37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? 39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. 40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? 41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?"

Yesu alishawaambia na tuvuke mpaka ng'ambo, haikujalisha njiani watakutana na shida kiasi gani au dhoruba kiasi gani wangefika ng'ambo kwasababu tu ni Yesu mwenyewe ndiye amesema. Yesu alisemalo ni lazima atalitimiza hakuna cha kuzuia kile anachotaka kufanya juu yako, mpaka dhoruba kali haikuweza kumshinda. Leo nataka ujiulize maswali yafuatayo:

1. Yesu amekwambia nini?
2. Wewe unasikia nini?
3. Unaona nini baada ya Yesu kumwambia?
4. Unafanya nini baada ya kusikia kutoka kwa Yesu?

Kwenye Biblia, Yesu amekuahidi ahadi nyingi sana, je unazijua?, jua sana nini Yesu amekwambia, maana ni hakika hilo alilokwambia atalitekeleza katika maisha yako, haijalishi leo una hali gani unapitia matatizo gani cha muhimu ni kukumbuka nini amesema kwa ajili yako.

Wanafunzi wa Yesu waliona dhoruba lakini Yesu aliona shwari kuu, Yesu aliona FURSA MBELE ya kuwaokoa, unaweza ukathani unalopitia ni shida kubwa sana lakini kwa Yesu hicho ni kitu kidogo sana na ni fursa ya kukuonyesha uweza wake unavyoweza kufanya makuu.

No comments:

Post a Comment