USIVIANGALIE VIONEKANAVYO BALI VISIVYOONEKANA
Maandiko: 2kor 4:5-18
Vionekanavyo ni vya kitambo kidogo tu bali visivyoonekana ni vya milele. Vitu vya hapa duniani (vionekanavyo) yasikuchanganye ukamuacha Mungu, bali kaza macho yako kwa Mungu mwenye uzima wa milele udumuo. Changamoto na shida za hapa duniani zisikuchanganye ukamuacha Mungu wako aliyekuumba bali mshike Yeye kwani utapata faida ya milele.
Katika kila hali unayopitia katika maisha yako tazamia kumuona Yesu Kristo akikuinua zaidi ya hapo ulipo, tarajia mambo makuu kutoka kwake, tarajia furaha na amani ya kweli kutoka kwake.
Mathayo 6:24-33, kwasabb tupo kwny mwili wa nyama, changamoto za maisha zipo lakini zisikutishe mpaka ukapata hofu ukaacha kuishi maisha matakatifu, bali muweke Mungu namba moja na hayo mengine utazidishiwa, Mungu atafungua milango mbayo kwa akili zako usingeweza kuifungua, Mungu atakupa mpenyo. Cha muhimu umtazame Yeye usiangalie shida zako, Yesu anaweza yote.
Ukimtazama Yesu Kristo maumivu ya maisha za maisha hayatakusumbua kwasababu atayaponya yote. Yakobo 1:2-4, 1Petro 1:6-7, 2Korintho 12:7-9, Neema yake yatutosha, hakuna shida iliyowahi kumshinda Yesu, weka imani yako kwake.
No comments:
Post a Comment