''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, August 18, 2019

UMEBARIKIWA TANGU SIKU ULIYOUMBWA

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Neno: Mwanzo 1:26-30

Mwanzo 1:26-30
"26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; 30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. 31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita."


Mungu alikuwa amashaumba vitu vingi siku za zote tano za mwanzo lakini vyote vyote alivyoviumba siku hizo za mwanzo hakuviumba vifanane na sura yake, bali siku ya siku ya sita kaona mwanadamu amuumbe kwa kufanana na sura yake. Mungu alitupa nafasi ya pekee sana mpaka akaamua atuumbe kwa kufanana nae. 

Kwahiyo alitukirimia nafasi ya tofauti sana, na hakuishia hapo tu (mstari wa 28) baada ya kutuumba tu akatubariki hapo hapo, lakini hakuishia hapo tena akatuongezea baraka  nyingine akatupa uwezo wa kuzaa na kuongezeka, uwezo wa kongezeka upo ndani yako tayari; kwamba tuzae matunda na tuongezeke, haijalishi sahivi una mtoto au bado lakini hiyo ni ahadi aliyotupa Mungu tangu mwanzo. 

Pia Mungu akatupa nguvu ya kutawala dunia, hapa Mungu alitupa uwezo mkubwa sana wa kutawala mazingira uliyonayo, haijalishi ni mazingira gani unapititia lakini tambua kwamba ndani mwako tayari Mungu amashaweka mamlaka ya kuyatawala ni wewe tu kuelewa hilo na kuchukua hatua. Kwahiyo kama kuna vitu kwenye maisha yako vinakusumbua ilimradi una Yesu ndani una uwezo wa kubadilisha, kuondoa vyote usivyopenda.

Mwanzo 5:1-5 , inaweka wazi pia kwamba baada ya Mungu kutuumba akatubariki sana. Kwahiyo hatutakiwi kuishi kama mtu uliyekata tamaa, Mungu wetu ametubariki sana sana na kutupa uwezo mwingi.

Yohana 17:20-21, Hapa pia Yesu baada ya Kumaliza kazi alituombea tena na kutubariki. Mpendwa Mungu ametubariki sana, unapoona mambo hayajakaa sawa, kumbuka hili kwamba umebarikiwa tangu ulivyoumbwa, na kama umebarikiwa tambua kwamba utafanikiwa tu katika maisha yako. Hutakiwi kukaa kama mtu va kawaida, wewe si mtu wa kawaida wewe umebarikiwa. SISI KAZI YETU NI MOJA NI KUISHI KWENDANA NA NENO LA MUNGU(KULIJUA NENO NA KULIIISHI).

No comments:

Post a Comment