''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, September 1, 2019

TEMBEA KATIKA KANUNI ZA YESU KRISTO

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: 1Yohana 1:7-9

1Yohana1:7-9
"Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

Kutembea katika kanuni za Mungu ni kitu cha muhimu sana maishani mwako. Kila mtu anapaswa unapaswa kuishi kama vile Mungu anavyotaka, Mungu anataka tuishi maisha ya Nuru, maisha matakatifu. Wanadamu hatuwezi kuishi maisha matakatifu kwa nguvu zetu,  ndio maana Mungu akamtuma mwana wake wa pekee Yesu Kristo ili kupitia Yeye wewe upate uwezo wa kishinda dhambi. Bila kumkubali Yesu Kristo maishani mwako hutaweza kuishinda dhambi, hutaweza kuacha dhambi, mpaka utakapokubali Yesu Kristo akusaidie.

Sasa ili Yesu Kristo aendelee kuishi maishani mwako, ili aendelee kuishi na wewe kukusaidia uishi maisha matakatifu, ni lazima ukubali kuishi kwa kanuni zake. Kanuni yake namba moja na ndio iliyo kuu ni Upendo, Umpende Mungu kwa moyo wako wote na pia umpende jirani yako. Ukimpenda Mungu utazishika amri zake, ukiamua kupenda Mungu hutaona uzito wa kumtumikia Yeye. Ukimpenda Mungu hitaona uzito kwa kusoma Biblia / Neno la Mungu wala kuomba. Ukimpenda Mungu kwa kumaanisha hutaona shida kumpenda jirani yako.

Kanuni nyingine kubwa, ni Unyenyekevu. Ili Yesu Kristo aendelee kuishi ndani mwako ni lazima uwe mnyenyekevu mbele zake na mbele za wanadamu. Kinyume cha unyenyekevu ni kiburi, Yesu Kristo hapendi kabisa mtu mwenye kiburi. Usiwe mtu wa kujihesabia haki, Mungu atakutapika, lakini ukijinyenyekeza chini ya mkono wake naye atakukweza kwa wakati wake, 1Petro 5:6. Mungu akuwezeshe kuishi katika kanuni zake.

No comments:

Post a Comment