Mhubiri: Mzee wa Kanisa, Leandri Kinabo
Maandiko: 1Samweli 4:12-22
Uwepo wa Mungu ni wa muhimu sana katika maisha yako, na unapopoteza uwepo wa Mungu ndani mwako utukufu wake unaondoka pia. Hapa Wana wa Israel walimuacha Mungu wakaacha kanuni zake wakawa wanaenenda kama wanavyotaka wao Mungu akawaacha. Kwakuwa walikuwa wanashinda vita kila mara wakadhani na wakati huo watashinda wasijua kwamba Mungu alishawaacha, wakapigana vita wakapigwa sana mpaka Sanduku la Bwana likachukuliwa.
Ni hatari sana kuishi bila Uwepo wa Mungu katika maisha yako. Wana wa Israel waliachwa na Mungu bila wao kutambua mapema, walizani kuwa Mungu yupo tu kumbe walipoacha kufuata kanuni za Mungu Mungu aliwaacha.
Hivyo hivyo kuna watu wanadhani ukiokoka ndio umemaliza ukianza kwenda kanisani basi ndio umemaliza unaanza kuwa mzembe kuomba, kusoma Biblia na kufanya kazi ya Mungu. Unaweza ukadhani wewe ni mtakatifu sana na ukajisahau, ukasahau nini Mungu anataka ufanye, nini kanuni za Mungu, ufanyapo hivyo uwepo wa Mungu utaondoka maishani mwako, ulinzi wa Mungu hautakuwepo. Mungu atakusaidia tu ukimrudia Yeye na kutubu dhambi zako.
Wana wa Israel walidhani kuwa Sanduku la Bwana haliwezi kuchukuliwa, lakini kwasababu waliuacha uwepo wa Mungu ndomana utukufu wake ukaondoka. Unaweza kuwa na jina la KiKristo, unaonekana mtakatifu lakini utakapo fanya dhambi tu uwepo wa Mungu hapo hapo unakuacha.
1Wakorintho 3:16-17 " Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi." Wewe ni hekalu la Mungu, unapomuacha Mungu na kukosa uwepo wake Mungu atakubomoa.
Galatia 6:7 "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."
Badilika leo, mrudie Mungu, Mungu nae atakurehemu.
No comments:
Post a Comment