''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 29, 2020

UTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko : 1Petro 1:13-24, Zaburi 1:1-6, Waebrania 12:14

1Petro 1:14-16 "Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."


Utakatifu ni kuiacha dunia na kumtumikia Mungu wako, mstari wa 15, Mungu anakuita uwe mtakatifu uachane na mwenendo wa mwanzo, mwenendo wa dhambi. Ishi maisha ambayo Mungu anayakubali ambayo ni ya utakatifu. Katika Mstari wa 17 inasema tutembee kwa hofu katika wakati wa kukaa hapa duniani, hapa duniani tunapita nyumbani kwenu ni mbinguni ambapo hatuwezi fika bila huo Utakatifu, Yakupasa uwe mtakatifu.

Chunguza mwenendo wako sasa, unapoingia na kutoka mwenendo wa maisha yako upoje? Rudi kwa Bwana leo. Hapa duniani sisi ni wapitaji hatutakaa siku zote duniani, kwahiyo andaa sehemu unayoenda. Katika mstari wa 23 inasema umezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyoharibika na mbegu hiyo ni Yesu Kristo.

Katika Zaburi 1:1- Mtu mtakatifu amelinganishwa na mti ulio kando kandi ya vijito vya maji ambao haukauki na uzaao kwa majira yake. Ukiona unakaa zaidi kwenye mabaraza ya wenye mizaha ujue Roho Mtakatifu ameondoka. Ukiwa ndani ya Yesu, Unakuwa kiumbe kipya ya kale yamepita. Inapaswa tuwe matakatifu kama Yesu alivyo mtakatifu

Unajitaidi mambo mengi lakini hufanikiwi kwasababu ya sio mtakatifu, wako watu wanafanya dhambi kwa siri sana, maisha ya jinsi hiyo utaaibika siku moja maana Mungu atakuweka wazi adharani kwasababu Mungu yupo kinyume na dhambi, sasa kwanini uaibike kwanini usimrudie Mungu kwa moyo wote. Uovu ulionao huwezi kumficha Mungu, tubu sasa!


Waebrania 12:14 "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"

Zaburi 24:3-5 "Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake."

Hakuna chochote kinyonge kitakachingia mbinguni maisha yako mwenendo wako lazima ubadilike, hebu mrudie Mungu kwa toba, leo hii kama Bwana Yesu akirudi akakukuta  hujatubu kwanini uingie kwenye hasara ya kubaki?, Bwana Yesu anarudi saa yoyote je akirudi utaenda? Je una sifa za kwenda na Yesu Kristo? Tubu sasa..

No comments:

Post a Comment