UJUMBE WA LEO: KUMGUSA MUNGU KIBINAFSI
-------------------------------------------------------
MAANDIKO: Marko
5:25-34, Luka 7:44-48
MHUBIRI: MRS. MASEMBO
-------------------------------------------------
Kumgusa Mungu ni kufanya kitu cha ziada kwa ajili ya Mungu,
ndio umeokoka lakini je? Unafanya kitu kipi cha ziada kwa ajili ya Mungu?.
Kuokoka peke yake hakutoshi unatakiwa
baada ya kuokoka ufanye kitu Fulani ambacho kitamgusa Mungu mojamoja.
Yule kahaba alimgusa Yesu kwa matendo yake, alimfuta Yesu
kwa nywele zake alimbusu miguu yake na kumpaka Yesu marhamu. Ndio Yule Simoni
alikaribisha Yesu lakini hakufanya zaidi ya hapo, Je? Leo umefanya kitu gani
cha zaidi cha kumgusa Yesu?.Tafuta leo
ni kitu gani utakacho kifanya ili umguse Yesu.
Yule mama aliyetokwa na damu miaka 12, aliamua kufanya kitu
cha ziada kwa kugusa vazi la Yesu kwa imani naye akapokea uponyaji wake. Aliamini kwamba hata akigusa tu vazi la Yesu
atapona. Unatakiwa kumgusa Yesu KIBINAFSI, ndio unaunda kanisani lakini Je? Umemgusa Mungu kibinafsi?
Kumbuka kwamba huyu mwanamke aliyetokwa na damu alikuwa
haruhusiwi kuchangamana na watu lakini aliposikia Yesu mtenda miujiza amekuja
hakujali kwamba ataonekana na mafarisayo lakini alikuwa tayari kwa chochote
kile ilimradi amguse Yesu. Usijali watu watasema nini juu yako wewe jitahidi
kufanya kitu ambacho kitamgusa Yesu.
Unaweza kumgusa Mungu kwa mali zako, au kwa nguvu zako kama
kufanya kazi nyumbani mwa Bwana kupiga deki kanisa, ni lazima utafute chochote cha
kufanya kwa Mungu ambacho kitamgusa Yeye. Ni jambo gani linalokutesa kwa muda
mrefu sasa, ingia gharama ya kufanya kitu kitakacho mgusa Yesu.
Fanya uamuzi leo na chukua hatua kama huyo mama alivyosema,
mwambie Mungu imetosha mimi kuendelea kukaa na shida hii halafu mguse kwa
kufanya kitu na Mungu atakujibu shida yako. Pia kwa kumtafuta Mungu kwa bidii
sana Mithali 8:17. ‘inawezekana
kubadilisha hali yoyote uliyonayo’
For sure, hili neno nami limenigusa sana, Je katika kizazi hiki ni watu wangapi wanamgusa Mungu kwa matendo yao, je matendo yetu kama kanisa la Bwana tunamgusa Mungu? For sure hatuna budi kukaa na kujitafakari tena kwa upya kwamba Je? Tunamgusa Mungu au tupo tu kawaida, and nothing extra we do???
ReplyDelete