UJUMBE WA LEO: KUMJUA YESU KIBINAFSI
------------------------------------------------------
MAANDIKO YA SOMO: Mathayo
16:13-20
MHUBIRI: Mch. MUSSA ELIAS
-----------------------------------------------
Yesu aliwauliza wanafunzi wake “Watu
hunena Mwana wa Adam kuwa ni nani?”, Simon Petro alijibu Wewe ndiwe Kristo,
Mwana wa Mungu alite hai. Je? Kwendana na maisha yako, Yesu ni nani kwako?.
Yesu ni mwamba kwahiyo akikaa kwako na weweukikaa ndani yake, utakuwa imara hata ukipita katika majaribu
magumu hutatetereka. Ili uishi maisha mazuri
ni lazima ujenge nyumba yako kwenye mwamba
Ukimjua Yesu kibinafsi hutatishwa
na malango ya kizimu. Unaweza kiuwa unatembea na Yesu lakini usimjue kibinafsi.
Wanafunzi wa Yesu walikaa na Yesu kwa miaka 3 lakini sio wote waliomfahamu Yesu
au kumuelewa vizuri, Yesu aliposema nitasulubishwa Petro akamwambia hutakufa lakini
Yesu akasema rudi nyuma wewe shetani. Petro kwa wakati ule hakujua malengo ya
Yesu ni nini, hakumfahamu Yesu kibinafsi. Pia Yesu aliwaambia wanafunzi wake
siku ya 3 yaani ya ufufuo kwamba atakuwepo Galilaya lakini cha kushangaza siku
ya 3 ilipofika wakaenda kumwangalia kaburini. Inaonyesha kuwa walikaa na Yesu
kwa muda mwingi lakini hawakuamini alichowaambia.
Hii inamaanisha kwamba unaweza
ukawa umeokoka vizuri tena una muda mrefu katika wokovu lakini usiwe unamjua
Yesu kibinafsi kwasababu husomi Neno la
Mungu pia huombi. Unahitaji kusoma
Neno la Mungu ili umjue Yesu kibinafsi, usisubiri kuja kulisoma kanisani.
No comments:
Post a Comment