''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 3, 2013

UJUMBE WA LEO: KWA JINA LA YESU SIMAMA UENDE!
-------------------------------------------------------------------------------
Maandiko: Matendo 3:1-16, Matendo 4:21-22

Kwa Jina laYesu simama uende! ni tangazo Petro alilompa yule kiwete aliyekuwa akikaa katika mlango mzuri wa kuingia hekaluni. Petro alimwambia yule kiwete "Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende."

Yule kiwete alikaa katika hali ya ukiwete kwa zaidi ya miaka 40, yawezekana na wewe umekaa katika tatizo au matatizo flani kwa muda mrefu mpaka umeyazoea umeyaona yamekuwa yako lakini leo Yesu anasema Simama Uende. Yawezekana ni ugonjwa wa kurithi au ni ugonjwa ambao madaktari wamekwambia hautibiki kama cancer au ukimwi lakini leo Yesu anakwambia simama uende uachane na hali hiyo, au inawezekana unaenda kanisani lakini hujaokoka na unazani kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila kutenda dhambi lakini leo badilisha mtazamo wako na usimame uondoke katika hali hiyo. Lakini inategemea na uamuzi wako leo wa kutii tangazo hilo au lah.

MAMBO MAWILI MAKUMBWA ALIYOFANYA YULE KIWETE

1. Kiwete alibadilisha mtazamo wake kuhusu udhahifu alionao, unajua kiwete alizoea kupewa pesa kwahiyo alivyo waona Petro na Yohana mtazamo wake ulikuwa ni kupata pesa kutoka kwao lakini petro alimwambia "Tutazame sisi" na kiwete akatii na akakubali kuwatazama akiwa na mtazamo mwingina sio wa kupata pesa bali kupata kitu.
Leo fika mahali ubadilishe mtazamo wako juu ya shida yako, toka katika mtazamo dhaifu, nani kakwambia kuwa Yesu hawezi kuponya ukumwi au cancer au magonjwa ya kurithi? Je! unazani huo ni mtazamo sahihi? Yesu anaweza YOTE jukumu ni lako kuamini hilo.

2. Kiwete alijihusisha katika kupokea muujiza wake. Kiwete alipoambiwa simama alikubali kusimama na akatii akasimama na akaamini kwamba hataanguka wala hakuweka mashaka. Amini Yesu kuwa anafanya. Fanya kinyume na ile hali uliyoizoelea kwa muda mrefu, fanya kitu ambacho ulikuwa huwezi kufanya, Uweza ulio katika Jina la Yesu Kristo ndio utakao badilisha hali uliyonayo.
Ni jukumu lako wewe sasa kuamini kuwa Yesu anaweza kukuondoa katika hali uliyonayo, na hali hiyo itakuacha, Amen.

No comments:

Post a Comment