''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, February 10, 2013

UJUMBE WA LEO: MUNGU ANAPENDEZWA NA KWELI ILIYO MOYONI.
-------------------------------------------------------------------------------------

MHUBIRI: Mzee wa kanisa, Dr. Mumghamba
Maandiko: Zaburi 51:1-12, Mathayo 15:3
 
Mungu anapendezwa na kweli iliyo ndani mwako tu na sio vitu vingine, Kweli iliyo ndani ya moyo wako tu ndiyo Mungu anayoiangalia. Mungu hataudharau moyo ulio pondeka na kunyenyekea mbele zake. Ndio unaweza kuwa unatoa sadaka sana au una bidii sana katika kufanya huduma fulani kama maombi lakini kama Kweli ya Mungu haipo ndani ya moyo wako ni kazi bure. 

Mathayo 15:8-9, watu wengi wamekuwa wanafiki bila kujua, kwa nje unaonekana kama uko moto kumbe ndani uko baridi, unasema umeokoka lakini kumbe unafanya dhambi kimya kimya. 
     Jiulize mwenyewe:
  • Je, ni kweli gani uliyobeba ndani ya moyo wako?
  • Je, unaenenda kama Yesu anavyotaka au kama wewe unavyotaka?, 
  • , Je, Mungu anapendezwa na maisha yako?, 
  • Je, una nini moyoni mwako?, 
  • Je, kazini au shuleni kwako wanajua utakatifu wako? 
  • jirani yako anaona matendo mema kutoka kwako?. 
Yeremia 17:8-10, ni Mungu peke yake ndiye anayejua vizuri moyo wako kuliko wewe unavyojua, kwahiyo mruhusu Mungu atawale moyo wako leo. Ufunuo 3:1-2, Unajina la kuwa hai lakini kiukweli kumbe umekufa, tubu leo na uanze maisha mapya na Yesu, na Yesu yuko tayari kukusamehe na kukaa ndani yako. Amua sasa kuishi maisha matakatifu mbele za Mungu, achana na dhambi za kufanya chini chini amua kweli kuishi na Yesu Kristo. Na ulinde sana moyo wako kuliko vyote uvilindavyo.

No comments:

Post a Comment