UJUMBE WA JUMAPILI: MUNGU ANA MPANGO MZURI KWA AJILI YAKO
----------------------------------------------------------------------------------
MAANDIKO: Yeremia 10:23, Isaya 30:19-27
MHUBIRI: Mch Meshark Mhini
---------------------------------------------------
Mungu alikuumba sio kwa ajili yako mwenyewe bali ni kwa
ajili yake hivyo basi mkabidhili leo mambo yako yote ili akuongoze kuyapangilia
kwendana na mapenzi yake. Ni kweli unapitia mapito flani flani magumu lakini
fahamu kuwa Mungu anafahamu kuwa unapitia katika hali hiyo, nab ado ana mpango
mzuri kwa ajili yako labda anaruhusu hayo ili akutengeneze uwe chombo chake
kizuri zaidi, kwahiyo usikate tamaa, kuwa mvumilivu, endelea kumuomba Mungu
naye atafanya kitu kizuri sana kwa ajili yako zaidi ya kile ulichotegemea.
Mungu ana mpango
mzuri leo kwa ajili yako, mpango wa kukutana na shida zako zote. Hapo katika
Isaya, Mungu aliwaambia wana wa Israel, ‘wewe hautalia tena’. Mungu anakwambia
leo hautalia tena, usilie tena Mungu ana mpango mzuri kwa ajili yako cha
muhimu, Kaa karibu na Mungu, Mwamini Mungu, Jitenge na uovu wa kila aina acha
dhambi kabisa, na utambue wewe bila Mungu si kitu wala huwezi kitu.
No comments:
Post a Comment