Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: 1Samweli 30:1-20
Daudi na watu wake walilia mpaka wakakosa nguvu ya kulia tena, lakini badae akajitia nguvu katika Bwana, akachukua hatua ya kumtafuta Bwana. Katika maisha ya hapa dunia, unaweza kupitia nyakati ngumu, nyakati za majaribu, nyakati za kupungukiwa ukalia sana, lakini je ni unafanya baada ya kulia sana?, hatua gani unachukua baada ya kupata matatizo? Daudu hakuishia tu kulia lakini alichukua hatua ya kumuomba Mungu. Unapopatwa na shida chukua hatua ya kumwambia Mungu, omba kwa Mungu kwa kumaanisha naye atasikia.
Daudi alimuomba Mungu akamuuliza kama akaiwafwatia atawapa? na Mungu akamjibu. Mwambie Mungu shida, Mungu yuko tayari kukusikia naye atajibu atakuonyesha njia ya kupita, atakuelekeza jinsi ya kufanya ili kuondokana na hitaji lako, atakupa majibu ya kweli. Chukua hatua ya kusonga mbele na kuongea na Mungu.
Acha kulia chukua hatua, Fahamu kuwa hakuna shida yoyote inayomshinda Mungu, Mungu wetu ni Mungu mwenye nguvu sana. Kuwa na muda mzuri wa kuomba, omba kwa bidii, ni lazima utenge muda wako wa kuwasiliana na Mungu wako vizuri na kumueleza, kumuuliza nini ufaye hatua gani uchukue. Mungu akubariki.
No comments:
Post a Comment